Hussein Makame, NEC .

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kujifunza uzoefu wa tendaji wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) ili kuimarisha utawala bora nchini.

Jaji Mst. Lubuva ametoa wito huo wakati akeleza uzoefu wake juu ya utendaji kazi wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Tume hiyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Alisema pamoja na TKU kukabiliwa na changamoto nyingi katika inatekeleza majukumu yake wakati huo lakini ilifanya kazi zake kwa ufanisi kutokana na malalamiko ya wananchi yaliyoshughulikiwa kwa wakati huo.

“Katika hali na mazingira ya Tume ya wakati huo, bila kusita nashawishika kusema kuwa Tume ya Kudumu ilianzishwa wakati ambapo si watu wengi kwa bahati mbaya Afrka ambao walijali haki za binadamu na utawala bora” alisema Jaji Mst. Lubuva.

Aliongeza kuwa itakuwa si kusifia kusema kuwa TKU ilifanya kazi nzuri katika kipindi chake cha miaka 32 kwani ulikuwa wakati ambapo Tanzania ndio ilikuwa imejikomboa kutoka utawala wa Kikoloni na ilijitahidi kuendesha shughuli za maendeleo kwa wananchi.

Hata hivyo alisisitiza kuwa walithubutu kwa mwalimu kuleta wazo la kuanzisha TKU ili kunusuru wananchi kutakona na madhila ya matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi na watendaji kwa wakati huo.

“Kwa upande mwingine Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ina kibarua kizito katika kutekeleza majukumu yake katika mazingira ya sasa ambapo tume hii si rahisi kuelezea kwa wananchi kwa nini isifanikiwe zaidi ya TKU” 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa akipokea tuzo ya Heshima ya Utawala Bora kutoka kwa Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Mhe. Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (katikati) akiwa amepokea Cheti cha Utambuzi wa Utumishi wake kwenye Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) kutambua mchango wake.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Tom Nyanduga na kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Mary Massay.
1. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva, akibadilisha mawazo na Wanasheria Wakuu wa Serikali Wastaafu wenzake Jaji Mst. Mark Bomani 1965-1976 na Jaji Mst. Joseph Sinde Warioba 1976 -1985.Jaji Mst. Warioba alitumikia nafasi hiyo kuanzia mwaka 1985 hadi 1993.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (wa tatu kulia) akiungana na kwenye picha ya pamoja na na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Viongozi wengine wa Serikali Wastaafu waliohudhuria maadhimisho hayo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...