Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman
akifungua Mkutano wa siku mbili wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki
kimataifa leo jijini Arusha. Mkutano huo umeandaliwa na Africa Group for
Justice and Accountability.
1.
Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa
unaojadili masuala ya Haki Kimataifa kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye
Majadiliano leo jijini Arusha. Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wamewakilisha nchi
za Senegal, Afrika ya Kusini, Sierra Leone, Uganda, Tanzania, Kenya, na
Botswana.
1 Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akishiriki
kwenye Mjadala kuhusu masuala ya Haki kimataifa leo jijini Arusha.
Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki
Kimataifa wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman
(Hayupo Pichani) wakati akifungua mkutano huo leo jijini Arusha. Wa kwanza
kushoto ni aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na
Mjumbe wa Africa Group for Justice and Accountability Mheshimiwa Catherine
Samba-Panza.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman
(Katikati) akijadiliana jambo na Mjumbe wa Africa Group for Justice and
Accountability na aliyekuwa Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa
ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Mheshimiwa Hassan Bubacar Jallow kabla ya
kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki kimataifa leo jijini
Arusha.
PICHA NA LYDIA CHURI-MAHAKAMA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...