Jumuiya ya watanzania na marafiki wa Northern California wametoa mchango wao wa kiasi cha Tsh milioni kumi laki mbili sabini na moja elfu na mia moja hamsini. (Tsh milioni 10,271,150/=) kusaidia serikali katika kukabiliana na wahanga pamoja na maafa yaliyotokana na tetemeko mkoani Kagera.

Shukrani ziwaendee wote walioweka mkono wao na nguvu zao katika kufanikisha hili zoezi bila kusahau chama cha watanzania eneo hili la ghuba (TCO) kwa kusaidia kuratibu zoezi zima na pia kuchangia kwa kiasi kikubwa.

Fedha zimetumwa katika account ya bank ya CRDB kama ilivyoelekezwa na serikali ili zifike katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera ambapo ndio shughuli zote za zoezi hili zinaratibiwa.

Katibu wa mkuu wa mkoa wa Kagera Thomas James Salala amethibitisha kiasi cha pesa hiyo kuingia katika account hiyo na kutoa shukrani kwa niaba ya mkuu wa mkoa. 

Aksanteni sana.

Erick Byorwango
Katibu Mwenezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...