Jumla ya watoto sita waliozaliwa wakiwa na vichwa vikubwa mkoani Tabora wamefanyiwa upasuaji huku wengine 30 wakipata maelekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali hiyo bila ya kuwa mzigo kwa jamii iliyowazunguka katika awamu ya nne ya kambi tiba za GSM Foundation zinazoendeshwa kea kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Upasuaji na Mifupa ya Muhimbili MOI.

Idadi hii inasababisha jumla ya watoto waliotibiwa na kambi tiba hizo zilizoanza mwezi Aprili mwaka huu na kupita zaidi ya mikoa 15  kufikia watoto 196 huku kambi ikiwa bado inaelekea kuifikia mikoa mitatu zaidi ya Tanzania Bara na baad ya halo kuelekea Visiwani Zanzibar mapema mwezi Novemba mwaka huu.

Akiongea na wanahabari kabla ya kufunga kambi tiba hiyo inayotembea na madaktari Bingwa wanne, amnesie wanne na mabwana usingizi wawili, Kaimu Mkuu wa kambi tiba hiyo Dk Hamis Shaaban amesema bado kuna changamoto ya uelewa kwa wazazi wenye watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa ambapo wengi wao bado hawaamini kwamba tiba za kitabibu zinaweza kumaliza tatizo la watoto wao.

“Wengi wao bado wanaamini kwamba tatizo hili ni la kulogwa hivyo huwaficha watoto wao kwa waganga wa kienyeji, na mpaka tunapowafikia tunakuta muda wa kuweza kuokoa afya na maisha yao kwa ujumla unakuwa umeshapita”, alisema Dk Shaaban

Kwa upande wake Afisa Habari wa GSM Foundation, Bw Khalphan Kiwamba amewaomba wananchi walioa mikoa ya Kagera, Kigoma, Rukwa na Zanzibar ambako kambi tiba hiyo inaelekea kujitokeza ili kuipata fursa hiyo ambayo hakuna hakika kwamba inaweza kutokea tena katika miaka ya karibuni.

“Gharama ya kumtibu mtoto mmoja mwenye  kichwa kikubwa ni karibia shilingi milioni moja za kitanzania, laciniĆ© GSM Foundation imelipia gharama zote za tiba kwh mikoa yote ya Tanzania kea mwaka huu na huenda mwakani tussle na kambi za namna hii. Kwa hiyo tujitahidi kuchangamkia fursa”, alisisitiza Kiwamba.
Dk Pascal Joachim akimsikiliza mzazi wa mtoto Seleman Said kabla ya kupatiwa matibabu katika kambi tiba ya GSM Foundation katika Hospitali ya Kitete Mkoani Tabora.
Madaktari wakiwa katika Kliniki.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwamri akiwa emembeba mmoja kati ya watoto waliohudhuria kambi tiba ya GSM Foundation.
Mtoto Mjema Gilbert akiwa kwenye foleni ya Kambi tiba ya GSM Foundation akiwa na Mama yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...