Asasi isiyo ya kiserikali ya Community Voices In Focus (CVF)  imezindua kampeni kwa jina BINTI WA KITAA eneo la Pakacha kata ya Tandale wilaya ya Kinondoni itakayodumu kwa mwaka mmoja yenye lengo la kuelimisha jamii ili kupunguza na kuondoa tatizo la mimba pamoja na ndoa za utotoni  nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa (CVF) Ndg. George David amesema kama mtanzania ameguswa na tatizo hili ambalo limedumu kwa muda mrefu katika jamii hata katika kipindi hiki cha utandawazi hivyo anaamini kupitia kampeni hii, elimu itawafikia walengwa kwa namna ya tofauti na licha ya kupunguza tatizo hili itasaidia kulimaliza kabisa.

"Inauma sana kuona nchi yetu inatajwa kati ya nchi 5 duniani  zinazotambulika kwa janga la mimba pamoja na ndoa za utotoni, hivyo ni dhahiri kuwa huu ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuhakikisha mabinti kwenye jamii yetu wanafikia malengo yao kwa wakati husika na sii vinginevyo" alisema  George.

BINTI WA KITAA  imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 17 sio tu kwa wale waliopo shuleni bali hata wale waliopo mitaani na inatarajiwa kuzuru mikoa zaidi ya 10 nchini huku ikiwa na agenda ya kuwafikia mabinti katika mitaa wanayoishi ili kuwapa fursa hata wazazi kuweza kushiriki katika kuwa sehemu ya ukombozi wa binti wa Kitanzania.

Kwa kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto zinazowapelekea mabinti kupata mimba na kuolewa zipo katika jamii hasa mitaani,hii ndio iliyosababisha kampeni hii kuzinduliwa mtaa wa Pakacha Tandale kwani.
Baadhi ya waliofanikisha uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa Kitaa wakiwa wanaonesha #tag  Binti ya Kitaa.
Baadhi ya akina mama wa Tandale pamoja na waendeshaji wa Kampeni ya Binti wa kitaa wakiwa katika uzinduzi
Baadhi ya wawezeshaji, na wakazi wa Tandale wakionesha Mabango ya Binti wa Kitaa
Picha ya pamoja  .Picha zote na Fredy Njeje/Story na Mwana Libeneke wa Funguka Live Dickson Mulashani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...