Kampuni ya uagizaji na uuzaji wa magari ya Japani ya Be Forward, ikishirikiana na Be Forward Tanzania, imetoa hundi yenye thamani ya dola za kimarekani 5000, ambayo ni sawa mifuko ya saruji 700, ikiwa na lengo la kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mauzo na Masoko wa kampuni hiyo, Musa Abbas alisema kuwa kampuni yake imeguswa kwa kiasi kikubwa na janga hilo la tetemeko la ardhi na kwa kushirikiana na Beforward Japan imekuwa kutoa msaada huo ili kusaidia ukarabati wa miumbo mbinu iliyoaribika ikiwemo makazi.

“Sisi kama Be Forward, tumeguswa kwa kiasi kikubwa na janga hili na leo hii tunakabidhi dola za kimarekani elfu 5000 zikilenge kununua mifuko ya saruji 700 ili kusaidia ukarabati wa miundo mbinu na makazi iliyoaribiwa na tetemeko hilo.“Tunatoa wito kwa makampuni mengine yaendelee kutoa michango ili kusaidia waathirika wa janga hili kwa bado hawajachelewa, tunawaasa wazidi kuchangia ili kuwapa ahueni waathirika wa janga hilo,” alisema Bw. Abbas.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu (Sera na Uratibu)katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Yokobety Malisa, akipokea msaada huo, alitoa shukrani kwa kampuni Be Forward kwa kuitikia wito wa Waziri Mkuu na kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.“Kwa niaba ya ofisi ya Waziri Mkuu, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Be Forward kwa kuitikia wito na kujitokeza kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea mkoani Kagera hivi karibuni.

“Msaada huu utasaidia kuleta ahueni kwa wakazi wa Kagera ambao makazi na miundombinu yao imearibiwa na tetemeko hilo kwa kiasi kikubwa,” alisema Bi. Malisa.Bi. Malisa hakikishia kampuni hiyo kuwa msaada waliyoutoa utawafikia walengwa na kutoa wito kwa watu na makampuni mengine kutoa misaada ili kusaidia waathirika hao wa tetemeko la ardhi.


Mkuu Mauzo wa Kampuni ya kuuza magari ya Be Forward. JP, Yush Gushiken, akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Yokobeth Malisa, mfano wa hundi yenye thamani ya dola za marekani 5,000 kwa ajili ya ununuzi wa mifuko 700 ya saruji kusaidia waathirika wa tetemeko la Kagera.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi Yokobety Malisa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Be Forward mara tu baada ya kampuni hiyo kukabidhi hundi yenye thamani ya dola za marekani 5,000 kwa ajili ya ununuzi wa mifuko 700 ya saruji kusaidia waathirika wa tetemeko la Kagera.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...