Waziri mkuu  Kassim Majaliwa  akipokea picha yenye sura yake kutoka kwa mwenyekiti wa kampuni  ya Ujenzi ya CRCC ya China Bw. Fengchao kulia ni katibu wa chama cha ushirikano na maendeleo kati ya china na Tanzania Bwana Joseph Kahama  ujumbe huo kutoka china ulifika ofisini kwa waziri mkuu  Magogoni jijini dar es salaam kwa mazungumzo ya kikazi nakutoa pole kwa tetemeko la kagera.
 Waziri mkuu  Kassim Majaliwa akiwa katika picha.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya CRCC ya China Bw. Fengchao Meng ambaye ameahidi kuwekeza kwa kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya mkoa wa Dodoma.

Mwenyekiti huo ambaye aliongozana na Mwenyekiti wa Kampuni nyingine ya Ujenzi ya CCECC ya China, Bw. Yuan Li pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha  Urafiki kati ya Serikali za Tanzania na China, Bw. Joseph Kahama .

Akizungumza na Bw. Meng leo (Jumatatu, Oktoba 10, 2016) ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesema kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni uendelezaji wa Makao Makuu Dodoma.

Aliongeza kuwa China na Tanzania ni marafiki wa muda mrefu na mataifa hayo yanashirikiana vizuri katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali hivyo Serikali inatarajia mengi kutoka kwenye kampuni hiyo kupitia kwa mwenyekiti wake Bw. Meng.

“Dodoma kuna fursa za uwekezaji kwenye sekta nyingi kama miundombinu, kilimo na viwanda. Mnaweza kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba za makazi, ofisi, huduma za kijamii na viwanda ,”

Kwa upande wake Bw. Meng amesema kampuni yake itaungana na Serikali katika kuboresha Makao  Makuu ya Serikali na inatarajia kutuma wataalam wake mkoani Dodoma kuangalia maeneo ya uwekezaji.

‘Nataraji tutakuwekeza katika ujenzi wa miundombinu, nyumba za makazi, ofisi, maeneo ya kutolea huduma za jamii na teknolojia zitakazowezesha upatikanaji wa maji safi na salama.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, OKTOBA 10, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera Serikali kwa kutoa fursa kwenye ujenzi. Lakini kwani hakuna kampuni binafsi za wazawa wa kuchukua hizi kazi?
    Je, hakuna kampuni za nchi nyingine kupata hizi tenda, ila ni wachina tu?
    Hivi NHC wanfanya nini ikiwa hii ndio shughuli yao au wao wapo zaidi kwenye kujenga magorofa na kuuza tu? Kwanini wasiwatumie baadhi ya wataalam wao wazawa kuchukua hizi kazi?
    Hivi sisi tunaweza nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...