THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Kampuni ya Metropolitan Tanzania yaadhimisha miaka 10 Huduma za Bima

Kampuni ya Metropolitan Tanzania ilianzishwa kutokana na Kampuni ya Metropolitan International ambayo inamilikiwa na MMI Holdings. Nchini Tanzania, Kampuni hii inayojihusisha na masuala ya Bima ilianza huduma zake rasmi Juni 7, 2016.

Ikiwa chini ya Kapuni ya Momentum Tanzania (PTY) LimMetropolitan Tanzania inaadhimisha miaka kumi yenye mafanikio katika utoaji wa huduma zake nchini, huku ikitangaza kuboresha huduma zake zaidi katika utoaji wa huduma za bima.

kizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katika hafla maalumu, Mkurugenzi Mtendaji wa Metropolitan Tanzania.. alisema kuwa miaka mitatu baada ya kuanzishwa kwa kapuni hiyo, walijikuta wakiwa katika orodha ya kampuni bora na zinazokua kwa haraka katika soko la bima nchini 

 “Tangu kupewa jina la Metropolitan Tanzania lililotokana na muungano wa Momentum and Metropolitan in 2013, kampuni hii imekuwa katika soko la bima nchini tangu wakati huo ikifanya vyema na ofisi zake zikiwa jijini Dar es Salaam, alisema Aliongeza kusema Hivi karibuni kampuni ya MMI ikiwa kama mwekezaji wa kigeni nchini imewekeza jumla ya mtaji wa shilingi za kitanzania bilioni 7.4. lakini kabla ya hapo Desemba 2105 mtaji wa kampuni hiyo ulikuwa shilingi za kitanzania bilioni 8.5”. K

wa mujibu wa Mkurugenzi huyo, jumla ya mtaji wa kampuni hiyo hadi sasa ni shilingi za kitanzania bilioni 16, hali ambayo inaifanya kampuni hiyo kuwa miongoni mwa kampuni zinazofanya vizuri katika soko la bima kwa kuwa na msimamo mzuri wa mtaji.

 “Kampuni hii inapoadhimisha miaka kumi ya huduma zake nchini, niwafamishe wadau wetu wote kuwa tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora na kujiimarisha zaidi kibiashara ili tuendelee kuwapo katika soko kwa mafanikio
Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na wageni waalikwa wakati wa sherehe fupi ya miaka kumi ya Metropolitan iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla fupi ya miaka kumi ya Metropolitan wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (hayupo pichani).