Kampuni inayotengeneza vinywaji baridi , SBC Tanzania Limited (Pepsi) imemkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa kiasi cha Shilingi milioni 50 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10 mwaka huu na kuua watu wapatao 16, kujeruhi wengine zaidi ya 200 huku likiacha mamia wakiwa hawana malazi, chakula na huduma nyingine za kijamii.

Mtendaji Mkuu wa SBC Tanzania Limited (Pepsi), Bw. Avinash Jha amesema kampuni yake imeguswa na janga hilo la kitaifa na linaungana na wadau wengine kuchangia msaada kwa waathirika hao.

“Tunaunga mkono jitihada za Serikali na Mheshimiwa Raisi John Pombe Magufuli kusaidia waliopatwa na janga hili. Tupo pamoja ilikuwafariji walioopoteza ndugu, jamaa au rafiki ikiwamo na kuharibikiwa kwa makazi, miundo na kusabisha wamia ya watu kukosa huduma za msingi za kijamii. Kampuni ya SBC Tanzania Limited (Pepsi), imekuwa ni sehemu ya jamii ya Watanzania kwa miaka mingi, ikitoa huduma mbalimbali kwa wakazi wa mikoa mbalimbali ukiwemo Kagera ”, aliendelea kusema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Bw. Jha aliyeambatana na maofisa kadhaa wa SBC Tanzania Limited (Pepsi), akiwemo mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa kampuni hiyo, Bw. Alexander Foti Gwebe Nyirenda amemwabia Mhe Waziri Mkuu kuwa “Hatuna budi kusadia jamii, sio tu kwa sababu ni wadau wetu na wanatuunga mkono kwenye biashara yetu ya vinywaji, bali ni kwa kuwa lazima tusaidie jamii inayotuzunguka, kwa kuonyesha moyo wa huruma na kutoa msaada.” amesema Jha,

“Kampuni yetu siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii, tukishirikiana na serikali yetu kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo elimu ili kuleta maendeleo,”

Akitoa mifano ya misaada ya Kampuni ya SBC Tanzania Limited (Pepsi), Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo amesema mwaka huu pekee wameshazawadia madawati zaidi ya 200 kwa shule ya msingi mkoani Dar es Salaam na kupitia ofisi ya mkoa wa Shinyanga wametoa Shilingi milioni 20 ili kutatua changamoto la madawati kwa wanafunzi wa shule.

Baada ya kukadidhi mfano wa hundi ya Shillingi milioni 50 ofisini kwa waziri mkuu Jha amesema kuwa hawataishia hapa kwani pam kampuni hiyo inafurahia ushirikiano mzuri na serikali pamoja na wadau wengine wanaopenda maendeleo ya taifa letu.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alishukuru uongozi wa kampuni hiyo na kusema kuwa msaada huo umefika wakati mwafaka kwani wakazi wa mkoa wa Kagera wanahitaji msaada wa kukarabati na kujenga makazi na miundo mbinu zingine.

“Nimefarijika sana kwa ushirikiano huu ambao mnautoa kwa serikali na kuonyesha moyo wa upendo. Serikali itahakikisha msaada huu unatumika ipasavyo na haitasita kuwachukulia hatua wale wote wenye nia ya kuihujumuna kusababisha msaada kutowafikia walengwa,” aliendelea kusema Waziri Mkuu Majaliwa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya SBC Tanzania Limited (PEPSI), Bw. Avinash Jha (tatu kulia) akimkabidhi Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (tatu kushoto) hundi ya Shilingi milioni 50 kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwenye kampuni ya SBC Tanzania Limited (PEPSI), Bw. Alexander Foti Gwebe Nyirenda (pili kulia) na Mkurugenzi wa Masoko Bw Fadi El Khalil.Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya SBC Tanzania Limited (PEPSI), Bw. Avinash Jha (tatu kulia) akimkabidhi Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (tatu kushoto) hundi ya Shilingi milioni 50 kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwenye kampuni ya SBC Tanzania Limited (PEPSI), Bw. Alexander Foti Gwebe Nyirenda (pili kulia) na Mkurugenzi wa Masoko Bw Fadi El Khalil.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa kampuni ya Pepsi mara baada ya makabidhiano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...