Pichani
kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie, akizungumza leo jijini
Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habaria,wakati kampuni hiyo
ikitangaza kuanza kwa
sherehe maalumu ya kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya
Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na
uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.Helene amesema
kuwa kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo
miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru
wateja wake na umma wa Watanzania kwa kuikubali bia ya Serengeti kama
chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa
nchini.
PIchani kulia ndio muonekano mpya wa bia
ya Serengeti ambayo imekuja na kauli mbiu mpya wa kinywaji hicho cha
“Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.” SBL imewakaribisha wateja wake na
wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi katika hafla ya
maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya Serengeti yatakayofanyika leo jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa na uongozi wa kampuni ya SBL, ilipokuwa ikitangaza kuanza
kwa sherehe maalumu ya kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia
ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana
na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.Helene amesema
kuwa kuonesha mafanikio ya bia
ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL
itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja wake na umma wa
Watanzania kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo
kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.
Kampuni
ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza kuanza kwa sherehe
maalumu kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti
Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi
upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.
Akizungumza leo
jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi
Mkuu wa SBL Helene Weesie, amesema mbali na kuonesha mafanikio ya bia ya
Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL
itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja wake na umma wa
Watanzania kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo
kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.
“Tunawashukuru wateja
wetu, wafanya biashara, wasambazaji, mashirika ya sekta binafsi,
serikali na wadau wote ambao kimsingi wametusaidia na kuwa
nasi katika safari yetu hii ya mafaniko,” amesema Weesie.
Bia
ya Serengeti Premium Lager ni ya kwanza kutengenezwa kwa kimea kwa
asilimia 100 hapa nchini ikiwa ni ubunifu wa Mpishi Mkuu mtanzania
aitwaye Winston Kagusa ambaye alichanganya mbinu ya utengenezaji wa bia
za kijerumani na vionjo vya hapa nchini kupata kupata kinwaji hiki
kinacopendwa na wengi.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, bia ya Serengeti ilizalishwa kwa mara ya
kwanza ikilenga kufikia sehemu ndogo maalumu ya soko lakini azma hii
ilibadilishwa na kuzalishwa kwa wingi kutokana na ongezeko kubwa la
mahitaji ya bidhaa hiyo jambo ambalo lilisababisha kuanzishwa uzalishaji
zaidi katika viwanda vya SBL vilivyoko Moshi na Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...