THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Kampuni ya TTCL kuendelea kuboresha miundombinu ya mawasiliano

 KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imesema itaendelea na utekelezaji wa kuboresha miundombinu ya mtandao wake wa simu za mezani, mkononi pamoja na huduma za data ili kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wake na kufikia kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano nchini. Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu 
 
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba alipokuwa akizungumza na wateja mbalimbali kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa huyo wa TTCL, alisema kuwa maboresho ya miundombinu yanayofanywa kwa sasa katika shirika hilo yanaliwezesha kukabiliana na changamoto zilizokuwepo awali na kuwapa wateja weke fursa ya kufurahia huduma mpya na za zamani zinazotolewa kisasa na kwa umahiri mkubwa hivi sasa. 
 
"Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inaendelea na utekelezaji wa uboreshaji wa miundombinu ya mtandao wa simu za mezani, simu za mkononi na huduma za Data ili tuweze kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wetu na kufikia kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano," alisema Waziri Kindamba. 
 
Aidha alifafanua kuwa TTCL inawaahidi wateja wake na taifa kwa ujumla kwamba itaendelea kutoa huduma bora, za uhakika na gharama nafuu katika kutengeneza mazingira mazuri ya kiteknolojia, kwani baada ya mabadiliko watumishi wake wameazimia kuongeza kasi ya kufanya kazi kwa bidii, uadilifu, ubunifu na uzalendo wa hali ya juu ili kwenda sambamba na mahitaji ya sasa na baadaye ya wateja wa sekta ya Mawasiliano.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba akizungumza na wateja wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki,ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Thomas Mushi (wa pili kulia) akipata picha na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Edwin Mashasi.