Na Daudi Manongi, MAELEZO.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora amesema kuwa kata 345 zimefaidika na mradi wa kuboresha miundombinu ya mawasiliano nchini na Serikali mtandao kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote.

Profesa Kamuzora amesema hayo katika Warsha ya Habari na Mawasiliano iliyoandaliwa na Benki ya Dunia ikishirikiana na Wizara hiyo ikizungumzia mafanikio ya mradi wa kuboresha miundombinu ya Mawasiliano nchini na Serikali mtandao.

“Kupitia Serikali mtandao tunataka huduma za serikali ziwafikie wananchi kokote walipo na tunafahamu sasaivi wananchi wengi wana simu za mkononi na hivyo tunataka huduma kama za manunuzi kama tenda za Serikali na usajili wa vizazi na vifo kuanzia sasa zipatikane kwa njia ya mtandao ,huduma hii itaongeza uwazi,ufanisi na ubora wa huduma katika shughuli mbalimbali za Serikali.”Alisema Prof Kamuzora. 

Pia Profesa Kamuzora amesema kuwa Mradi huo ulilenga kufikisha mawasiliano vijijini na maeneo ambayo ni magumu kufikika na wafanyabiashara na ilipata mkopo wa masharti nafuu wa dola milioni 100 kutoka Benki ya Dunia ambao umesaidia kutoa ruzuku kwa makampuni mbalimbali ya simu ili yaweze kujenga minara kwenye maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara na hivyo kufanikiwa kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 2. 

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia anaeshughulikia masuala ya Habari na Mawasiliano Bi.Boutheina Guermazi amesema kuwa wataendelea kusaidia sekta ya mawasiliano nchini kwa kuwa ni muhimu katika maendeleo ya nchi yeyote na hivyo hawatasita kutoa misaada mbalimbali iwapo watahitajika kufanya hivyo.

Akizungumzia mafanikio ya mradi huo amesema kuwa kwa sasa kumekuwa na maboresho makubwa katika mawasiliano na upatikanaji wa vifurushi vya intaneti kwani sasa vimekuwa vya bei ya chini tofauti na mwanzo ambavyo vimesaidia upatikanaji wa mawasiliano katika maendeleo ya nchi.
Katibu Mkuu  Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustine Kamuzora akiwa na mwakilishi kutoka Benki ya Dunia anaeshughulikia masuala ya Habari na Mawasiliano Bi.Boutheina Guermazi wakati wa warsha ya Habari na Mawasiliano  ikizungumzia mafanikio ya mradi wa kuboresha miundombinu ya Mawasiliano nchini na Serikali mtandao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...