THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari Prof. Elisante Ole Gabriel kufungua kongamano kuhusu mabadiliko ya uendeshaji wa klabu za soka nchini

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel anatarajiwa kufungua kongamano kuhusu mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji katika klabu za soka nchini.
 
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Jumamosi Oktoba 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuhusu mifumo ya kiuendeshaji ambayo klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zipo mbioni kuingia na limeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
 
Kongamano hilo litaanza saa nne na nusu asubuhi na litarushwa live (mubashara) na kituo cha televisheni cha Azam kupitia chaneli yake ya Azam Two.Dhamira kubwa ya kongamano hilo ni kupata maoni ya kitaalamu kuhusu mifumo hiyo, ambapo Simba ipo mbioni kuingia mambo ya hisa, wakati Yanga utaratibu wa kukodishwa.
 
Baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ni namna ya kuendesha klabu za soka kibiashara, uwekezaji, mambo ya hisa na masuala ya uthamini kukiwa na watalaamu kutoka taasisi mbalimbali nchini.
 
Pia kutazungumzwa umuhimu wa mabadiliko katika klabu hizo na harakati za kuzibadili zilivyoanza miaka ya nyuma na matokeo yake yalivyokuwa.
 
Lengo ni kujadili kitaalamu bila ushabiki wa namna yoyote kwani nia ni kujenga na kuimarisha soka na michezo kwa ujumla hapa nchini na ndiyo sababu tumealika wataalamu wa kada mbalimbali, viongozi wa zamani wa soka kwa tofauti na baadhi ya wadau wa soka.
 
Nawasilisha,
 
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
21/10/2016