Na Daudi Manongi,MAELEZO 

Kiwanda cha Biotec Product kilichopo kibaha mkoani Pwani ambacho kinamilikiwa kwa ubia baina ya Serikali za Tanzania na Cuba kimekusudia kuzalisha lita milioni 2 za dawa za viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu waenezao ugonjwa wa malaria nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa katika kiwanda hicho.

“Kiwanda hiki kitasaidia katika vita yetu ya kupambana na malaria kwa kuwa ni miongoni mwa magonjwa yanayowasumbua Watanzania na Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kuwatibu wagonjwa” alisema Waziri Ummy .

Waziri Ummy alisema dawa zinazotengenezwa kiwandani hapo zitaisadia tatizo hili na sekta ya Afya kwa kuwa uwezo wa Serikali ni kuzalisha lita milioni 2.5 kwa mwaka na wakati kiwanda hicho kinaweza kuzalisha lita milioni 2 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa katika Watanzania 100, watanzania 14 wanapatwa na ugonjwa wa malaria. Aliongeza kuwa dawa hizo zina uwezo kuua viuadudu hivi katika hatua za mwanzo za kuzaliwa kwa mbu na hivyo uzalishaji huo utapoanza utasaidia kupunguza gharama za kutibu malaria, kununua vyandarua na dawa za kuua wadudu wa mbu. 
Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa Mhe.Salvador Valdes Mesa(kushoto) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(katikati) wakimskiliza Meneja Teknolojia wa kiwanda cha Biotec Product Bi.Lourdes Gonzalez kinachozalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani. Picha na Daudi Manongi,MAELEZO .

Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Mlingi Mkucha wakati makamu uyo alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.Kushoto kwa makamu wa Rais wa Cuba ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu.

Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha Biotec Product ambacho kinazalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria Bw.Alejandro Torres kilichopo Mkoani Pwani. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...