THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KUMBUKUMBU

OMUTWALE Paschal Rutaihwa Kakiziba
13 JULAI 1935 – 28 OKTOBA 2004

Baba yetu mpendwa umetimiza mwaka wa 12 tangu ulipotwaliwa na Bwana. Picha yako inatukumbusha uwepo wako tulipokuwa sote hapa duniani, na hasa ukarimu, upendo, upole, uchangamfu na wingi wa busara.

Ni vigumu kukubali kwamba haupo nasi lakini hatuna budi kuamini kwamba uko nasi kiroho kwa vile tunaye Mungu ambaye anaendelea kututia nguvu kila iitwapo leo. Busara zako na ucheshi wako vinazidi kutuimarisha kila siku na tunaendelea kuzingatia maneno yako uliyokuwa ukihimiza juu ya kuwa na upendo na umoja katika familia huku tukiendelea kumtumaini Mungu wetu ambaye amekuita kwake.

Mke wako Mary-Hilda Kakiziba, rafiki yako Galita, watoto wako, wajukuu, wakwe zako, dada zako, kaka zako na wadogo zako, ndugu, marafiki na majirani wanakosa ucheshi na ushauri wako na wanakukumbuka daima. MISA YA KUMBUKUMBU ITAFANYIKA JUMAPILI, OKTOBA 30, 2016, SAA 3 ASUBUHI KWENYE KIGANGO CHA MT. ANTHONY WA PADUA, BOKO, DSM.

Tumaini letu linajengwa na neno lisemalo: ”Umevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo umeumaliza na imani umeilinda” (2Tim. 4:7) Tunakuomba Ee Bwana uendelee kuipumzisha roho yake mahali pema peponi, AMEN.