Na Fatma Kassim, Zanzibar.

Waziri wa Afya Zanzibar, Mahmuod Thabit Kombo amesema kuwa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ina nafasi kubwa ya kufanya uchunguzi ambao unasaidia kutatua matatizo mbalimbali kiafya katika jamii.

Amesema kutokana na kuwa Bodi hiyo inawalinda wananchi na mambo mbalimbali yanapelekea madhara ni vyema kufanya kazi kwa uwadilifu na kuishauri Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufanya kazi kwa jitihada zote ili kuepusha matatizo ya kiafya kwa jamii.

Akizindua Bodi ya Ushauri ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Waziri wa Afya ameitaka bodi hiyo  kuandaa mipango madhubuti itakayosaidia kuondosha mapungufu inayowakabili Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Amesema kutokana na kuwa maabara hiyo inafanya uchunguzi wa mambo mbalimbali ikiwemo vyakula,vinywaji na dawa za binaadamu pamoja na kudhibiti kemikali zinatumiwa viwandani na majumbani hivyo amewataka kufanya kazi kwa mashirikiano na taasisi mbalimbali ikiwemo bodi ya chakula dawa na vipodozi na shirika la viwango.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dk Yussuf Nuhu  Pandu amesema watahakikisha wanafakazi  kwa mujibu wa sheria zilizowekwa ili kuweza kufanikisha maabara ya Mkemia Mkuu  wa Serikali kufanyakazi zake kwa uadilifu.

Amesema kutokana na kazi za Maabara ni kulinda afya za Wazanzibar pamoja na mazingira yao kwa kuchunguza ubora wa chakula na kemikali watafanya kila jitihada kuona mambo hayo yanafanyika .

Nae Mkemia Mkuu  wa Maabara ya Serikali Dk Slim Rashid Juma amesema wameweza kupata mafanikio mbalimbali ikiwemo kuwa na sheria ya maabara namba 10 ya mwaka 2011 inayoipa maabara hadhi ya wakala wa Serikali.

Mafanikio  mengine ni Serikali kuwapatia majengo matatu katika eneo la Maruhubi Unguja  na jengo jengine eneo la Madungu Pemba kwa matumizi ya maabara.

Amesema licha ya mafanikio hayo pia wanakabiliwa na changamoto na uchakavu na uchache wa vifaa na mashine za kufanyia uchunguzi pamoja na uchache wa kemikali ambalo linashusha utendaji wa kazi za maabara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...