Waziri wa mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe (pichani juu), amempongeza Balozi Vo Than Nam wa Vietnam anayemaliza kipindi chake nchini, kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi kati ya Vietnam na Tanzania kwa kiwango cha juu.
 Akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 71 ya uhuru wa Vietnam kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana jioni iliyohudhuriwa na idadi kubwa ya mabalozi nchini, waziri huyo alisema uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni ya Vietnam ya Halotel katika sekta ya mawasiliano ni moja ya mafanikio makubwa ya mahusiano ya nchi zetu mbili.
Amesema milango iko wazi kwa makampuni zaidi kutoka Vietnam kuwekeza chini katika sekta mbalimbali na kuongeza kuwa uzoefu ambao Vietnam imeupata katika mageuzi yake ya uchumi kutoka uchumi wa kilimo hadi wa viwanda ni chachu kwa Tanzania inayofuata njia hiyohiyo.
Akimkaribisha Waziri huyo aliyekuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo, Balozi Vo Than Man aliwasifu Watanzania kwa moyo wa ushirikiano na kuahidi kuendeleza mahusiano kati ya nchi zetu mbili.
 Balozi wa Vietnam Mhe. Vo Than Man

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...