Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiagana na mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ambaye amemaliza ziara ya siku 3 ya kikazi nchini.

.....................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ameondoka nchini mchana huu baada ya kumaliza ziara ya kiazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Lengo la ziara hiyo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ni kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba hasa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya,utamaduni,michezo na utalii.

Katika sekta ya utalii, Serikali ya Cuba imeahidi kuisaidia Tanzania katika kuendeleza utalii katika fukwe pamoja na kubadilishana uzoefu na wataalamu wa hapa nchini katika sekta hiyo ili kusaidia kuongeza pato la taifa kupitia shughuli za utalii nchini.


Aidha kwenye sekta ya viwanda Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana katika ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kutengenezea madawa ya binadamu nchini.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ameagwa na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kuhitimisha ziara yake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimsindikiza mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ambaye amemaliza ziara ya siku 3 ya kikazi nchini.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...