THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAKONDA ATOA MILIONI 10 KWA ALIYETOBOLEWA MACHO.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Said Ally, ambaye ametobolewa macho hivi karibuni,pichani kati Mkewe Zara Sudi mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandish wa Habari.

Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii.
SIKU chache mara baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa kosa la kumtoboa macho ndugu, Said Ally wa Buguruni kwa Mnyamani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda ameamua kuendelea kumsaidia kijana huyo katika hatua zake za zote za matibabu na mtaji wa Shilingi Milioni kumi.

Akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kijana huyo kufika katika ofis za mkoa , Makonda alisema kuwa mara baada ya kufanyika uchunguzi na madaktari Bingwa wa Muhimbili imeonekana kuwa bado Said atoweza kupata tena nafasi ya kuona tena hivyo anahitaji matibabu ya ziada.
“Serikali ya mkoa imetoa gari ambayo atatumia kwa kipindi chote akiwa anaenda kupatiwa matibabu na shughuli zingine ambazo atakuwa anafanya mpaka hapo atakapokuwa sawa”alisema Makonda.

Kwa upande Ndugu Said Ally amesema kuwa anawashukuru madaktari kwa juhudi zote walizofanya na shukrani kubwa sana ziende kwa Gea Habibu wa Clouds Media na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa moyo wake aliounyesha kwa kujitoa kwa hali na mali.

“Kiukweli nimeona Mungu akiwa katika upande wangu kwa msaada ninaondelea kupata kutoka kwa mkuu wa Mkoa na watu wa Clouds na madakatari naomba mungu aweze kuwapa maisha marefu” alisema Said.
Makonda alimaliza kwa kusema kuwa Serikali ya mkoa inandaa utaratibu kwa ajili ya watu wengine ambao wanahitaji kujitolea kumsaidia Said hivyo jumatatu atatangaza rasmi.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kumsaidia Bwana Said Ally ambaye alitobolewa machi jijini Dar es Salaam.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. HK Anasema:

    Kwanza Pole sana Bw. Said Ally kwa yote yaliyokukuta. Pongezi za dhati na za pekee kwa Mh. Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Bw. Paul Makonda. Kusema kweli tangu madhila na mithihani hii imkute ndugu yetu Bw. Said Ally, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh. Paul Makonda, amekuwa ni faraja na msaada mkubwa sana kwa ndugu yetu Bw. Said Ally, ameweza kuonyesha juhudi zake binafsi na hata za wadhifa wako akiwa kama Mkuu wa Mkoa na mwenye kila sababu ya kuwajali, kuwathamini na kuwatumikia wananchi wa Mkoa wako. Binafsi nakupongeza sana kwa juhudi na jitihada zako za dhati unazozifanya day in day out na khasa kwa tukio hili lililowagusa wengi la kutobolewa macho hadi kupelekea upofu kwa ndugu yetu Bw. Said Ally. tunashkuru sana kwa kiasi cha fedha ulichoweza kumsaidia na usafiri ili aweze kujikimu na kumsaidia katika maisha yake ya kila siku hadi hali yake itakapokuwa sawa na ya kuridhisha. Mwenyeez Mungu atakulipa jaza yako huko usoni twendako mara 'Saba wa Sabini'. Tunakuombea kila la kheri na Mola akulinde katika kila jambo na akuongoze kwa kila mema na kukuepusha na mabaya yote, pia akujaaliye siha njema na ari ya kuzidi kuwatumikia wananchi wa Mkoa wako na Taifa kwa jumla.