Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa kadri iwekenavyo.

Hayo yamesemwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakati akiongea na wazee na watu wenye ulemavu alipotembelea kituo cha wazee na watu wenye mahitaji maalum cha Fungafunga kilichopo Mkoani Morogoro.

“Kundi hili ni moja kati ya makundi yaliyokatika hatari kubwa sana na kwa kiasi kikubwa ni kundi ambalo limekuwa likisahaulika sana na kuwafanya kukosa mahitaji muhimu wanayopaswa kuyapata hivyo rai yangu kwa Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu”. Alisema Mama Janeth.

Pia Mama Janeth alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli inatambua kuwa wazee ni rasilimali na hazina kubwa katika kukuza uchumi wa nchi hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu wasiojiweza wanapata huduma zote muhimu.

Aidha, Akiongea wakati wa kukabidhi msaada wa Mchele kilo 875,Unga Kilo 875, Sukari Kilo 175, Maharage Kilo 350 na Mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi boksi 1 Mama Janeth aliwataka viongozi wa kituo hicho kuhakikisha chakula hicho kinawafikia walengwa kama ilivyopangwa..
Mwenyekiti wa Wazee wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw. Joseph Kaniki. Akimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa msaada wa chakula na kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo kwani kusaidia wazee ni kulisaidia taifa pia.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiwaaga baadhi ya Wazee na watu wenye mahitaji maalum katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw.Rashid Omar akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli hotuba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...