Na Editha Karlo wa 
Globu ya Jamii,  Kagera

MAMA mmoja na watoto wake wanne wakazi wa kijiji cha Nyamilanda kata ya Kyebitembe wilaya ya Muleba Mkoani kagera wamefariki dunia jana baada ya kula chakula aina ya ugali unaosadikiwa kuwa na sumu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamilanda Trasias Baltromeo amesema watu hao waliofariki ni mama na watoto wake wanne ambao walikula ugali majira ya saa tisa mchana na kuanza kutapika na hatimaye kufariki dunia wakipelekwa Kituo cha Afya Kimeya kilicho jirani na kijiji hicho

Baltromeo amewataja waliofariki kuwa ni mama wa watoto Julitha Julius (35) Haujeni Julius (14) Superius Julius (12), Gabriel Julius (4) na Paschazia Julius mwenye umri wa miezi sita.
Mwenyekiti huyo alisema katika tukio hilo mama aliandaa mboga aina ya dagaa na kwenda kwa mama mkwe wake nyumba jirani kutafuta unga wa muhogo na walipomaliza kula yeye na watoto wake wakaanza kutapika na kuanza kuhangaika hatimaye wananchi wakafika lakini juhudi za kuokoa maisha yao hazikuzaa matunda.
"Nilipofika nilikuta hali ni mbaya wakitapika na kuamua kwenda kutoa taarifa polisi Kyebitembe lakini walipofika wakati wanawakimbiza hospitali ndogo ya kimeya wakawa wamefariki watoto wanne na mama yao”Alisema Mwenyekiti.
Tukio la Kifo kama hilo limetokea mwaka jana kata ya Kasharunga tarafa ya Kimwani jimbo la Muleba kusini wilayani humo ambapo watu saba wa familia moja walikula chakula chenye sumu na kuokoka watu watatu pekee wanne walifariki dunia.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi ameongea na mtandao huu naye pia amekiri kupokea taarifa hiyo na kwamba hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusishwa na vifo hivyo lakini uchunguzi wa wataalamu wa afya unaendelea ili kujiridhisha na kutambua aina ya sumu iliyotumika hadi watu hao wakapoteza maisha yao.
Mkuu wa wilaya ya Muleba mhandisi Richadi Ruyango amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba jopo la wataalamu wa afya na jeshi la polisi limekwenda kituo cha Afya Kaigara na Hospitali ya Rubya kufanya uchunguzi kwa miili ya marehemu hao.
Mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi katika tarafa ya7 kimwani kuwa makini na vyakula wanavyokula kwani hilo ni tukio la tatu la familia kula vyakula vyenye sumu na kupoteza maisha kijijini hapo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...