THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mama wajawazito waaswa kuhusu ulaji wa matunda na mboga za majani

Na Mwandishi Wetu

Asilimia kubwa ya wanawake walio katika hali ya kupata ujauzito nchini wanakabiliwa na hatari ya kujifungua watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi kutokana na tabia ya kutopenda kula matudda na mboga za majani hivyo kukosa virutubsho muhimu mwilini.

Dk Hamis Shaabani daktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu  kutoka Taasisi ya mifupa(MOI) ameyasema hayo wakati wa zoezi la ufungaji upasuaji wa vichwa vikubwa na migongo wazi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma
Bi Anastazia Mtilili mkazi wa kijiji minyinga wilayani Kibondo akimuangalia binti yake Tedia Mwesiga baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa katila hospital ya rufaa ya Kigoma na madaktari toka MOI chini ya ufadhili wa GSM Foundation.

Dk Hamis alisema kuwa utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI mwaka 2002 unaonyesha zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi na kati yao 500 pekee ndiyo wanaoweza kufika hospital na kupatiwa matibabu.

Akizungumzia chimbuko la maradhi hayo Dk Hamisi alisema kuwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi wanaweza kuzaliwa nacho au kupata siku chache baada ya kuzaliwa.

"Kwa wale wanaozaliwa na maradhi hayo ni kwasababu ya upungufu wa virutubisho ambavyo mama mjamzito anatakiwa avipate kabla ya kushika mimba  virutubisho hivyo vinapatikana  kwenye matunda, mboga za majani, mayai na vyakula vyote vyenye protini, pia maradhi ya mgongo wazi husababisha watoto kupooza na kushindwa kutumia miguu yao"alisema
Daktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo kutoka MOI Dkt Khamis Shaabani (wa katikati)akimpa maelezo ya mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa Kaimu Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Samweli Mtenga.

Alisema mpaka sasa kwa Mkoa wa Kigoma jumla ya watoto 48 walihudhuria kliniki na  wameshawafanyia upasuaji jumla ya  watoto nane wenye vichwa vikubwa sita na wawili wa mgongo wazi.

Ofisa habari wa GSM Foundation Khalfani Kiwamba alisema kuwa taasisi yao iliamua kudhamini matibabu ya maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi baada ya kuelezwa changamoto mbalimbali za matibabu ya maradhi hayo na uongozi wa Taasisi ya MOI.


BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Kama mwanamke anajaribu kupata mimba inabidi aanze kunywa FOLIC acid 400 mcg- kila siku mpaka alau wiki ya 12 ya ujauzito. Kama mwanamke huyu alishawahi kuzaa mtoto mwenye kichwa kikubwa au mgongo wazi basi dozi ya folic acid ni 5 mg kila siku, dozi hii kubwa itumiwe pia kwa kina mama wenye kisukari, wanaokunywa dawa za kifafa au wenye BMI > 30. Wajameni tutapunguza kuzaliwa kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
    Dr Bitozi.