Na Mwandishi Wetu

Asilimia kubwa ya wanawake walio katika hali ya kupata ujauzito nchini wanakabiliwa na hatari ya kujifungua watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi kutokana na tabia ya kutopenda kula matudda na mboga za majani hivyo kukosa virutubsho muhimu mwilini.

Dk Hamis Shaabani daktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu  kutoka Taasisi ya mifupa(MOI) ameyasema hayo wakati wa zoezi la ufungaji upasuaji wa vichwa vikubwa na migongo wazi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma
Bi Anastazia Mtilili mkazi wa kijiji minyinga wilayani Kibondo akimuangalia binti yake Tedia Mwesiga baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa katila hospital ya rufaa ya Kigoma na madaktari toka MOI chini ya ufadhili wa GSM Foundation.

Dk Hamis alisema kuwa utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI mwaka 2002 unaonyesha zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi na kati yao 500 pekee ndiyo wanaoweza kufika hospital na kupatiwa matibabu.

Akizungumzia chimbuko la maradhi hayo Dk Hamisi alisema kuwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi wanaweza kuzaliwa nacho au kupata siku chache baada ya kuzaliwa.

"Kwa wale wanaozaliwa na maradhi hayo ni kwasababu ya upungufu wa virutubisho ambavyo mama mjamzito anatakiwa avipate kabla ya kushika mimba  virutubisho hivyo vinapatikana  kwenye matunda, mboga za majani, mayai na vyakula vyote vyenye protini, pia maradhi ya mgongo wazi husababisha watoto kupooza na kushindwa kutumia miguu yao"alisema
Daktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo kutoka MOI Dkt Khamis Shaabani (wa katikati)akimpa maelezo ya mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa Kaimu Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Samweli Mtenga.

Alisema mpaka sasa kwa Mkoa wa Kigoma jumla ya watoto 48 walihudhuria kliniki na  wameshawafanyia upasuaji jumla ya  watoto nane wenye vichwa vikubwa sita na wawili wa mgongo wazi.

Ofisa habari wa GSM Foundation Khalfani Kiwamba alisema kuwa taasisi yao iliamua kudhamini matibabu ya maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi baada ya kuelezwa changamoto mbalimbali za matibabu ya maradhi hayo na uongozi wa Taasisi ya MOI.


BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kama mwanamke anajaribu kupata mimba inabidi aanze kunywa FOLIC acid 400 mcg- kila siku mpaka alau wiki ya 12 ya ujauzito. Kama mwanamke huyu alishawahi kuzaa mtoto mwenye kichwa kikubwa au mgongo wazi basi dozi ya folic acid ni 5 mg kila siku, dozi hii kubwa itumiwe pia kwa kina mama wenye kisukari, wanaokunywa dawa za kifafa au wenye BMI > 30. Wajameni tutapunguza kuzaliwa kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
    Dr Bitozi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...