Mkurugenzi
Mkazi wa Marie Stopes, Anil Tambay (katikati) akiongea na waandishi wa
habari kuelezea juu ya maadhimisho ya miaka 40 kwa kutoa huduma bure za
uzazi wa mpango na uchunguzi wa kansa ya mlango wa kizazi kama
maadhimisho ya miaka 40 ya Marie Stopes International. Maadhimisho hayo
yanatarajia kufanyika Novemba 2-4, 2016 kwenye kliniki na hospitali zake
zote nchini Tanzania.
Marie
Stopes Tanzania itatoa huduma za uzazi wa mpango na uchunguzi wa kansa
ya mlango wa kizazi bure kuanzia tarehe 2 hadi 4 Novemba kwenye kliniki
na hospitali zake zote nchini kama sehemu ya kuadhimisha miaka 40 ya
Marie Stopes International, na hivyo kuongeza idadi ya akina mama ambao
wamewezeshwa kuwa na maamuzi juu ya mustakabali wa maisha yao wa kupata
watoto kwa utashi na si kwa kubahatisha.
Marie
Stopes Tanzania ni sehemu ya Marie Stopes International, shirika la
kimataifa linalojihusisha na kutoa huduma za afya ya uzazi na
lilianzishwa mwaka 1976. Katika wiki inayoanzia Oktoba 31, tutakuwa
tuaadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Maries Stopes International.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...