Na Is-haka Omar, Zanzibar.

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wameshauriwa kuondosha mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) katika Katiba ya Zanzibar ya Mwaka mwaka 1984.

Ushauri huo umetolewa na Katibu  wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa Kamati Maalum ya NEC, CCM Zanzibar,  Hamad Yussuf Masauni katika Majumuisho ya ziara yake ya kuimarisha uhai wa Chama huko katika Ukumbi wa Amani Mkoa wa Mjini, Unguja.

Alisema huu ndio wakati mwafaka wa kuondosha mfumo huo kwani hauna tija katika maendeleo ya nchi badala yake ukiachwa itakuwa ni fursa kwa wapinzani kurudi tena katika serikali baada ya kufanyika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.

Alieleza kwamba nia ya CCM kukubali kuingia katika mfumo wa Serikali ya Umoja wa kitaifa (SUK) ni kushirikiana na vyama vya upinzani katika mipango ya maendeleo ya nchi pamoja na kumaliza siasa za chuki, hali ambayo CUF haikutaka kubadilika hivyo hakuna haja ya kubakisha mfumo huo katika Katiba ya Zanzibar.

Masauni aliwasihi Wawakilishi wa CCM kuhakikisha wanalinda kwa vitendo  maslahi ya Chama kwa kuandaa taratibu zote za kisheria kwa kufuta kipengele ndani ya Katiba kinachoeleza uwepo wa mfumo huo.

Alisema hatua ya mwisho itakuwa kurudi kwa wananchi kupiga kura ya maoni ya kukubali ama kukataa kuendelea na SUK, jambo ambalo kwa sasa ni rahisi kwani wananchi wengi hasa wafuasi wa CCM hawataki kuendelea na serikali hiyo.

“ Huu ni wakati mwafaka wa kuifuta CUF katika siasa za Zanzibar kwani hatuwezi kuendelea kuwa na ushirikiano na Chama kinachojali maslahi binafsi pamoja sera za utengano badala ya kuwaunganisha wananchi.
 Akizungumza Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa Kamati Maalum ya NEC, CCM Zanzibar,  Hamad Yussuf Masauni , na wafusi wa CCM katika mkutano wa majumuisho katika ziara yake aliyofanya Wilaya za Amani na Mjini Kichama Zanzibar.
Baadhi ya wafuasi wa CCM wakifuatilia kwa makini mkutano wa majukuisho ya Ziara ya Masauni uko katika ukumbi wa Mkoa wa Mjini kichama uliopo Amani Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...