THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAWAZIRI UGANDA NA TANZANIA WATEMBELEA ENEO LITAKAPOJENGWA GATI ITAKAYOTUMIKA KUPAKIA MAFUTA KUTOKA UGANDA KWENYE MELI

Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni wametembelea eneo la Chongoleani mkoani Tanga ambako kutajengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali ili kusafirishwa. 

Mafuta hayo yatapakiwa kwenye Meli hizo baada ya kusafirishwa na Bomba kutoka Hoima nchini Uganda kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi. 

Akiwa katika eneo hilo Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda aliwaeleza wananchi wa eneo hilo kuwa nchi ya Uganda inaishukuru Tanzania kwa kukubali Bomba hilo lipite katika ardhi ya Tanzania suala ambalo litakuwa na faida mbalimbali kwa Wananchi ikiwemo mabadiliko ya kiuchumi. 

Alisema kuwa lengo ni kuona kuwa mradi huwa huo unaanza kazi mwaka 2020 na ndiyo maagizo ambayo Marais wa nchi mbili wameyatoa kwa watendaji wanaosimamia Mradi huo wa Bomba la Mafuta. 

Mhandisi Muloni alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kujiandaa kikamilifu kwa fursa za kiuchumi kwani watekelezaji wa mradi watahitaji huduma mbalimbali kama za chakula, malazi na usafiri hivyo kupitia utoaji wa huduma hizo wananchi nao watapata kipato. 

Pia alizishukuru Sekta Binafsi za Uganda na Tanzania kwa kuwa tayari kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa akitolea mfano kampuni ya GBP ya Tanzania ambayo imeonesha nia ya kununua hisa katika kampuni itakayoanzishwa kwa ajili ya usimamizi wa Bomba hilo la Mafuta. 

Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Saba kushoto) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni (wa Nane kushoto) wakiwa katika Kata ya Chongoleani mkoani Tanga ambako kutajengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali baada ya kusafirishwa na Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda. 
Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tano kulia) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni (wa Nne kulia) wakisalimiana na mmoja wa Wananchi katika Kata ya Chongoleani mkoani Tanga ambako kutajengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali baada ya kusafirishwa na Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda
Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto mstari wa Mbele) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni (wa Pili kushoto mstari wa mbele) wakitoka katika eneo la Chongoleani mkoani Tanga baada ya kukagua sehemu itakayojengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali baada ya kusafirishwa na Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda.