Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, Mboni Masimba (kushoto) akizungumza na Caroline Mwaipungu ambaye ni Mtangazaji wa 102.5 Lake Fm Mwanza kuhusu Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.

Na BMG
Konagamano hilo limelenga kuwahamasisha wanawake kujikomboa kiuchumi ambapo wanawake mbalimbali waliofanikiwa kiujasiriamali, kibiashara na kielimu watakuwepo kuzungumza na wanawake Jijini Mwanza ambapo kiingilio itakuwa elfu 40 tu na utapata elimu, burudani pamoja na chakula.

"Atakuwepo Shekha Nasser ambaye ni mmiliki wa Shear Illusion na Mwanzilishi wa Manjano Foundation ambaye amefanikiwa kwenye biashara, atakuwepo Mkandarasi Maida Waziri ambaye amekuwa mkandarasi na amefanikiwa pamoja na Biubwa Ibrahim ambaye ana Kampuni inaitwa Namaingo Agri_Busness Agency ambayo inawawezesha watu mbalimbali katika masuala ya kilimo na wengine wengi". Amefafanua Masimba.
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, Mboni Masimba akiwa ndani ya 102.5 Lake Fm Mwanza akizungumzia Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu ndani ya Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, Mboni Masimba (kushoto) akizungumza na Caroline Mwaipungu ambaye ni Mtangazaji wa 102.5 Lake Fm Mwanza kuhusu Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...