THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MBUNGE LEMA AZUA TAHARUKI UZINDUZI WA UJENZI WA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO JIJINI ARUSHA LEO.VURUGU kubwa zimeibuka baina ya mkuu wa mkuu wa mkoa Arusha Mringo Gambo na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya buruka nje kidogo ya jiji la Arusha.

Vurugu hiyo zimeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho gambo kuvuruga ratiba iliyokuwa imepagwa na waandaaji wa hafla hiyo ambapo kwa mujibu wa ratiba iyo ilikuwa imepagwa kuwa hotuba ya mkuu wa mkoa ingetanguliwa na waandaji wa shughuli hiyo akiwemo waandaji wa hafla hiyo,wafadhili pamoja na mbunge Lema.

Kabla ya vurugu hizo mkuu wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexzanda Mnyeti swala ambalo liliibua mzozo mkubwa kwa wananchi walikuwa wamefika kushuudia tukio hilo la uzinduzi wakiwemo wafadhili waliofadhili mradi ambao ni shirika la kuhudumia afya ya mama na mtoto (maternity Afrika ).

Baada ya kuanza kuhutubia mkuu huyo wa mkoa akielezea historia ya mradi huo ikiwe upatikanaji wa eneo la kujenga mradi wa hospitali hiyo gafla mbunge lema alipo simama na kupinga hotuba hiyo hiyo na kudai imejaa upotoshwaji na siasa ndani kwani yeye ndie aliyetafuta eneo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo kutoka katoka kampuni ya mawala Advocate na sio kweli eneo hilo limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala ya mda mrefu .
Picha ikionyesha wa kushoto mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anatulizwa na mchungaji Wilfred Mlayi ,Wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa anatulizwa na mfadhili wa Mradi huo ambaye ni daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na Mtoto Duniani Edru Broun
Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto ambaye akupenda kutaja jina lake akiwa anamuomba mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kutulia na kumuaacha mkuu wa mkoa aendelee kutoa hutuba.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Kuna Maoni 7 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Neno moja tu: aibu!!

 2. Mbele Anasema:

  Kama kulikuwa na ratiba ya uzinduzi, kwa nini haikufuatwa? Hilo tukio linahitaji taarifa na ufafanuzi zaidi. Nimeona video mtandaoni inayoonyesha kuwa kulikuwa na tatizo kubwa. Labda wenye taarifa zaidi watatuletea.

 3. Anonymous Anasema:

  Shame to our leaders hamuwezi kusirtiri hisia zenu za kisiasa .

 4. Anonymous Anasema:

  Hivi huyu mkuu WA mkoa Si anatembea na polisi...kwanini asingewaamrisha wamkamate kisha wamtoe baada ya sherehe... Maana mbunge Ni raia Tu polisi nao hawajui kazi zao nadhani

 5. Anonymous Anasema:

  Dah ile tafiti inayosema katika kila watanzania wanne mmoja ni kichaa .nahisi ni kweli tena ukweli mtupu

 6. Anonymous Anasema:

  Huyu mbunge nafikiri hasiruhusiwe kufika mahali popote atakapokuwa mkuu wa mkoa maana hii ni aibu kubwa mno.Vingenevyo apatikane mkuu wa mkoa ambaye ni mwanachama wa Chadema

 7. queen Anasema:

  Ukisema kuwa mbunge asiruhusiwe kwenda mahara popote alipo mkuu wa mkoa utakuwa unakosea kwa sababu Mkuu wa nkoa nae ana mapungufu yake ndio maana Lema hataki kukubaliana na hali hiyo ya utumiaji wa mabavu