VURUGU kubwa zimeibuka baina ya mkuu wa mkuu wa mkoa Arusha Mringo Gambo na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya buruka nje kidogo ya jiji la Arusha.

Vurugu hiyo zimeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho gambo kuvuruga ratiba iliyokuwa imepagwa na waandaaji wa hafla hiyo ambapo kwa mujibu wa ratiba iyo ilikuwa imepagwa kuwa hotuba ya mkuu wa mkoa ingetanguliwa na waandaji wa shughuli hiyo akiwemo waandaji wa hafla hiyo,wafadhili pamoja na mbunge Lema.

Kabla ya vurugu hizo mkuu wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexzanda Mnyeti swala ambalo liliibua mzozo mkubwa kwa wananchi walikuwa wamefika kushuudia tukio hilo la uzinduzi wakiwemo wafadhili waliofadhili mradi ambao ni shirika la kuhudumia afya ya mama na mtoto (maternity Afrika ).

Baada ya kuanza kuhutubia mkuu huyo wa mkoa akielezea historia ya mradi huo ikiwe upatikanaji wa eneo la kujenga mradi wa hospitali hiyo gafla mbunge lema alipo simama na kupinga hotuba hiyo hiyo na kudai imejaa upotoshwaji na siasa ndani kwani yeye ndie aliyetafuta eneo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo kutoka katoka kampuni ya mawala Advocate na sio kweli eneo hilo limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala ya mda mrefu .
Picha ikionyesha wa kushoto mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anatulizwa na mchungaji Wilfred Mlayi ,Wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa anatulizwa na mfadhili wa Mradi huo ambaye ni daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na Mtoto Duniani Edru Broun
Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto ambaye akupenda kutaja jina lake akiwa anamuomba mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kutulia na kumuaacha mkuu wa mkoa aendelee kutoa hutuba.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Neno moja tu: aibu!!

    ReplyDelete
  2. Kama kulikuwa na ratiba ya uzinduzi, kwa nini haikufuatwa? Hilo tukio linahitaji taarifa na ufafanuzi zaidi. Nimeona video mtandaoni inayoonyesha kuwa kulikuwa na tatizo kubwa. Labda wenye taarifa zaidi watatuletea.

    ReplyDelete
  3. Shame to our leaders hamuwezi kusirtiri hisia zenu za kisiasa .

    ReplyDelete
  4. Hivi huyu mkuu WA mkoa Si anatembea na polisi...kwanini asingewaamrisha wamkamate kisha wamtoe baada ya sherehe... Maana mbunge Ni raia Tu polisi nao hawajui kazi zao nadhani

    ReplyDelete
  5. Dah ile tafiti inayosema katika kila watanzania wanne mmoja ni kichaa .nahisi ni kweli tena ukweli mtupu

    ReplyDelete
  6. Huyu mbunge nafikiri hasiruhusiwe kufika mahali popote atakapokuwa mkuu wa mkoa maana hii ni aibu kubwa mno.Vingenevyo apatikane mkuu wa mkoa ambaye ni mwanachama wa Chadema

    ReplyDelete
  7. Ukisema kuwa mbunge asiruhusiwe kwenda mahara popote alipo mkuu wa mkoa utakuwa unakosea kwa sababu Mkuu wa nkoa nae ana mapungufu yake ndio maana Lema hataki kukubaliana na hali hiyo ya utumiaji wa mabavu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...