Na Fredy Mgunda,Iringa.


Mbunge wa Jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto amegawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu za Jimbo hilo kwa lengo la kukuza vipaji vya wanamichezo na kuwandeleza ili wawe wachezaji bora hapo baadae.

Mwamoto ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Kilolo katika ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.

Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo vya Michezo, Mwamoto amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni kutokana na ahadi yake yeye kama Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao kuwapatia vifaa hivyo huku baadhi yao pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.

“Niliahidi kuleta vifaa vya Michezo kwa kila Kata.Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa nan leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mwamoto.Mwamoto ameongeza kwa kusema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.

“Mimi nimecheza mpira kwa mafanikio ndio maana hadi saizi,kwa hilo mimi najua kuwa michezo ni ajira rasmi hivyo mtu kama unakipaji kitumie kipaji chako vizuri”. Mwamoto.Amesema kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo
Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo
Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya wanawake wa kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...