Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii Mkuranga 

Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega ameungana na wananchi wa kijiji cha tundu,kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo ufyatuaji wa matofali kwa ajili zahanati mpya ya kijiji hicho.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha tundu baada kushiriki kufyatua tofali wa kijiji cha tundu kata ya Bupu , Ulega amesema nia yake ni kuona maendeleo yanapatikana Mkuranga yote.

Ulega amesema amefanya mikutano katika kata 25 na sasa katika ziara ya kijiji kwa kijiji pamoja na kitongoji kwa kitongoji nia kuangalia maendeleo kutokana wilaya ya mkuranga kuwa nyuma kwa maendeleo. Ulega amesema katika kufanya kazi amedhamiria kutatua changamoto ya elimu, maji ,barabara pamoja na afya ambpo changamoto hizo zikitatulika mkuranga itakuwa imesogea kwa maendeleo.

Mbunge huyo ametoa mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kufyatua tofali ya zahanati ya kijiji cha tundu. Amewataka walimu kuendelea kuwa na moyo wa kuwafundisha wanafunzi kutokana wilaya hiyo kuwa na elimu chini. Amewataka walimu wa shule ya sekondari bupu kuondoa sifuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka huu.

Wananchi wamemtaka mbunge kuondoa kwa kushirikiana wilaya kuondoa ng'ombe pamoja mfumo wa stakabadhi ghalani. Amesema kabila la Wazalamo na Wandengeleko kusomesha watoto kwa ajili ya maendeleo kutokana dunia ya sasa inahitaji watalaam.

Ulega amesema kuwa changamoto zilizo katika kata ya Bupu ni maji pamoja na miundombinu ya barabara hivyo vinatakiwa kupatiwa ufumbuzi ili waondokane na changamoto hizo. Mbunge huyo ameahidi kutoa Bati 50 katika shule mpya inayojengwa katika kitongoji cha kikonga kutokana watoto wa kitongoji hicho wanatembea kilomita sita.

Ulega amesema changamoto zilizopo wilaya ya mkuranga zinatakiwa zitatuliwe kutokana na kuomba kazi ya kuwatumikia wananchi.

Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa amebeba tofali alilofyatua kwa  mkono wake akipeleka sehemu ya kuhifadhi ili likaushwe na jua katika kijiji cha Tundu panapotarajiwa kujengwa Zahanati ya Tundu leo katika ziara yake kukagua maendeleo ya Wilaya hiyo.

Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Kiiiji cha Maamudi Mpela leo katika ziara yake kutembelea wananchi pamoja na kuwashukuru pamoja na kuwasikiliza kero zao leo mkoani Pwani. Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akishiriki katika ufyatuaji wa tofali kwa ajili ya zahanati mpya itakayojengwa katika kijiji cha Tundu leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake kukagua maendeleo wilaya hiyo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...