THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MBUNGE WA RUFIJI AHAHIDI KUWASAIDIA WAKINAMAMA WAJAWAZITO WANAOKABILIWA NA CHANGAMOTO YA KUJIFUNGULIA NJIANI

NA VICTOR  MASANGU, RUFIJI.

BAADHI ya wakinamama wajawazito wanaoishi katika vijiji vya  Mbunju na Mbambe vilivyopo kata ya Mkongo. Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya muda mrefu ya kujifungulia wakiwa  njiani kutokana na kuwepo kwa umbali mrefu kutoka makazi wanayoishi hadi kufika katika zahanati au  kituo cha afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Wakinamama hao wametoa kilio chao wakati walipotembelewa na mbunge wa jimbo la Rufiji ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi yenye  lengo la kuweza kusikiliza changamoto  mbali mbali zinazowakabili wananchi wake  pamoja na  kero zao  ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mikakati ya kuleta chachu ya maendeleo.

Zarau Kiambwe  Tabia Athumani,pamoja na Suzan Masela  ni miongoni mwa wakinamama hao wanaokabiliwa na changamoto hiyo,walisema  wakati mwingine wanapata wakati mgumu hususan nyakati za usiku kutokana na kukosa usafiri hivyo kuwalazimu kujifungulia njiani hali ambayo inahatarisha uhai wa kupopteza maisha yao ukizingatia na gharama za usafiri wa piki piki ni kubwa hivyo wanashindwa kuzimudu kutoka na kutokuwa na kipato chochote.

Aidha wakinamama hao wamemuomba Mbunge wa jimbo hilo la Rufiji kwa kushirikianana serikali ya awamu ya tano kuliingilia kati suala hilo ili kuweza kuwasaidia wananchi kwa  kuwajengeaa  zahanati pamoja na vituo vya afya vilivyvyo karibu na maeneo wanayoishi ili kuweza kupata huduma ya matibatu kwa urahisi bila ya  usumbufu.

 Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mbunju na Mbambe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuwatembelea kwa ajili ya kuweza kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
 Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na baadhi ya wanakijiji hicho kwa ajili ya kuweza kujadili kero zinazowakabili.
 Mbunge wa Rufiji akifurahia jambo baada ya mzee maarufu kijijini hapo kumpa pongezi za dhati kwa kuhudi zake anazozifanya katika kuwataumikia wananchi wa jimbo hilo.