THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MFALME MOHAMMED VI WA MOROCCO AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA MSIKITI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

  Mfalme Mohammed  VI wa Morocco akibusu Masahaf kabla ya kumkabidhi Waziri Mkuu Kasim Majaliwa katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti kwenye eneo la BAKWATA Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016.  Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abukary Zubeir. Jumla ya Masahaf 10000 zilikabidhiwa na Mfalme huyo
 Mfalme Mohammed  VI wa Morocco na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016
 Mfalme Mohammed  VI wa Morocco na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016
Mfalme   Mohammed VI wa Morocco,  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Rais Mstaafu Alhaj  Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Bilal wakiwa katika hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa msiki uliofnywa na Mfalme Mohammed wa Morocco kwenye  eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salam Oktoba 25, 2016.  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. HK Anasema:

    Masha Allah!. Jazaqallahu Khayr kwa yote aliyoyakubali kutukidhia Mfalme Mohammed VI wa Morocco, khusuana na hilo la ujenzi wa Masjid (Mskiti), basi In Sha Allah, jaza yake ataikuta kesho huko usoni twendako. Hakika mambo mithli ya hayo ndizo hizo 'Swadaqatin'jariya' tuhimizwazo kujitolea endapo hali na uwezo vinarukhusu. Kadhalika nimshkuru na kumpongeza kwa dhati Mh. Rais wetu Mh. John Pombe Joseph MAGUFULI kwa jitihada zake za dhati na za kipekee kabisa katika kuhakikisha watanzania wana kila sababu ya kupata maendeleo ya kila hali nchini katika nyanja zote za kimaisha pasina kujali wala kubaguwa tofauti zozote zile, ima za kidini, kikabila, rangi ,kisiasa, kiitikadi n.k. Kwa kweli amekuwa msatari wa mbele kwa hali na mali na hata kama ni kwa kujitolea muhanga, almuradi kuhakikisha kujengeka kwa Tanzania mpya itakayoongozwa na gurudumu la maendeleo ya kiuchumi khususan katika uchumi huu wa viwanda ambao utaambatana na maendeleo takriban katika kila sekta nchini. Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake. Ibariki Afirka na Dunia kwa jumla.

  2. Anonymous Anasema:

    Kabla hajaondoka jamani muombeni ajenge chuo Kikuu kikubwa huko kanda ya ziwa woote tumebanana Udom nna UDSM . Tutakuwa tumeweka balance ya nguvu . Elimu dunia ni ufunguo wa maisha .