Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI leo tarehe 27 Oktoba, 2016 ameondoka Jijini Dar es Salaam na kuelekea Zanzibar.

Katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed VI ameagwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyeambatana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed VI aliyewasili nchini tarehe 23, Oktoba 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli na pia viongozi hao wameshuhudia utiaji saini wa mikataba 21 inayohusu ushirikiano wa Tanzania na Morocco katika masuala mbalimbali ya kiuchumi.

Baada ya kumaliza ziara ya kiserikali ya siku tatu, Mtukufu Mohammed VI anaendelea na ziara binafsi hapa nchini.
  
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Oktoba, 2016.
ano1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akajadiliana jambo na Mfalme wa Morocco Mohamed VI kabla ya kuagana nae katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
ano2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
ano3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mfalme wa Morocco Mohamed VI kabla ya kuagana nae katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
ano5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mfalme wa Morocco Mohamed VI kabla ya kuagana nae katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...