THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF UMEENDELEA KUWAFIKIA WATU WENGI KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI (PSS)

Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wake wa uchangiaji wa Hiari (PSS) umeendelea kuyafikia makundi mbalimbali kujiunga na mpango huo. 

Hayo yamesemwa na  Afisa Mwendeshaji  kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary alipokuwa akitoa maelezo na mafunzo juu ya mfuko huo na wafanyakazi wa  Hoteli ya  Heritage iliyopo Jijini Dar es salaam  ambapo pamoja  na kutoa maelezo juu ya mfuko huo na kutoa  elimu ya juu ya mpango huo wa uchangiaji wa  hiari ambapo  mwanachama atatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 ,  atakuwa huru kuchagua muda wa kuchangia kutegemea kipato chake huku kiwango cha chini kikianzia Shilingi 10,000 ambayo mwanachama anaweza kulipia kupitia benki na huduma za simu.

Bwana Hadji alisema kuwa mpango huo wa hiari unakaribisha raia na mtu asiye raia bila kusahau mjasiriamali na mfanyakazi wa serikali  na kuongeza kuwa  mwanachama anayejiunga katika mfuko huo huweza kupata mafao ya aina sita ambayo ni; Fao la Elimu, Fao la Ujasiriamali, Fao la Uzeeni, Fao la Kifo, Fao la Ugonjwa/Ulemavu, Fao la Kujitoa, na Fao la Matibabu.

Akifafanua kuhusu Fao la Matibabu, Bwana Hadji alisema kuwa kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari wanashirikiana na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo mwanachama ataweza kupatiwa huduma bure katika hospitali na maduka ya madawa yaliyosajiliwa na NHIF kote nchini.

“Mwanachama anaweza kuwasajili pia wategemezi wake watano na kuendelea kupata mafao yetu bila shida yoyote,” alisema Hadji

Wakizungumza kwa nyakati mbalimbali wafanyakazi hao walionesha kufurahia unafuu wa mfuko huo na kuwataka PSPF kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wananchi wengi wajiunge kwa kuwa hupoteza fedha nyingi ambazo wangeweza kuziokoa kwa kujiunga na mfuko huo.

Aidha Hadji aliwaambia wafanyakazi  hao kuwa PSPF ina wawezesha  wanachama wake na jamii kwa ujumla kumiliki nyumba zilizopo Dar , Morogoro, Tabora, Mtwara, Shinyanga na Iringa ambapo wataweza kununua kwa mkopo au malipo ya mara moja pamoja na mikopo ya viwanja vilivyo sehemu mbalimbali nchini.


Afisa Mwendeshaji  kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary akiwaeleza wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage juu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF ikiwa ni pamoja na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) ambapo mtu yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 anaweza kujiunga na kunufaika na mafao mengi.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Hoteli ya Heritage wakiwa wanasikiliza kwa makini somo kutoka kwa Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary kuhusu mafao yatolewayo na mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA