Ally Daud-MAELEZO.
MFUMUKO wa bei wa umeshuka kwa asilimia 4.5  mwezi Septemba kutoka asilimia 4.9 ya mwezi Agosti mwaka huu kutokana na kupungua kwa upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi uliopita.

Hayo yamebainishwa na  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Ephraim Kwesigabo (Pichani)wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

Kwesigabo amesema kuwa kushuka kwa mfumuko wa bei kumetokana na kupungua kwa kasi ya upandajiwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali ikilinganishwa na Mwezi Agosti .
“Mfumuko wa bei mwezi Septemba umeshuka ukilinganisha na mwezi Agosti kutoka asilimia 4.9 hadi kufika asilimia 4.5 kutokana na kushuka kwa upandaji wa bei za bidhaa na huduma”. Alisema Bw. Kwesigabo.

Aidha aliongeza kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji Baridi vimepungua hadi kufika asilimia 6.0 kutoka asilimia 7.0 mwezi agosti mwaka huu.

Kwesigabo amesema kuwa ushukaji huo wa bei za vyakula na vinywaji baridi umetokana na kupungua kwa kasi ya bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoisha kwa mwezi Septemba mwaka huu.

Mbali na hayo Kwesigabo amesema kuwa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania imefikia shilingi 97.4 katika kununua bidhaa na huduma kwa mezi septemba ikilingfanishwa na shilingi 96.83 mwezi Agosti.

Aidha Mkurugenzi Kwesigabo amesema kuwa anawaomba wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa Ofisi za takwimu Za Mikoa wakati wa ukusanyaji wa takwi,u mbalimbali kwa maendeleo ya nchi yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...