DJ wa Maisha Basement, Ally Suleiman (DVJ Ally B) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa anatarajia kuzindua Mixtape ya Fresh From Kitaa Vol. 2 itakayofanyika Oktoba 9, mwaka huu Pale Maisha Basement Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Kulia ni Godwin Elia Dj (Godo).

Amesema kuwa Mixtape hiyo itakuwa ni mwendelezo wa Mixtape kwa miezi mingine itakayoendelea.

Pia amesema kuwa Mixtape hiyo itakuwa ni muunaniko wa nyimbo kali za wasanii hapa nchini pamoja na wasanii wa nje ya nchi ikiwa ni kuwaburudisha  mashabiki wa Mziki na kuwapa fursa ya kuzisikiliza live(Mbashara) yeye akiwa ndiye DJ wa kazi hiyo.

DJ Ally B amesema kuwa Mixtape Vol. 2 ameiandaa kwa utofauti sana kutokana na marekebisho makubwa ya maoni ya mashabiki wa Mziki waliyoyatoa.
Amesema kuwa katika uzinduzi huo kiingilio kitakuwa cha kawaida na cha shilingi elfu kumi pia kwa mashabiki wa kwanza kufika watajipatia CD ya Mixtape bure ili wakaisikilize nyumbani.
 Meneja wa kitengo cha Mawasiliano wa Maisha Basment, Robart Salehe katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na uzinduzi wa Mixtape Vol.2 katika Clabu ya Maisha Basement jijini Dar es Salaam. Kushoto ni DJ wa Maisha Basement, Ally Suleiman (DVJ Ally B) na Kulia ni Godwin Elia Dj (Godo) 
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...