THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MJADALA WA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WAENDELEO MJINI DODOMA CHINI YA KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ikiendelea na majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kushoto) akijibu hoja mbalimbali za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akisisitiza jambo kwa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson (kushoto) akifafanua jambo wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.