Huenda ukiambiwa utaje wanyama hatari sana duniani utakimbilia kwa simba ama chui kwa haraka......
 Nyegere ama Honey badger ni miongoni mwa wanyama hatari zaidi duniani, kwa tarifa yako tu hata nyoka, chui na simba huufyata kwa Nyegere ..............Nyegere ndio mmoja kati ya wanyama wasioogopa kitu chochote duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda. Na yeye hategemei mob/kuchangia mande kwani ni mmoja wa wanyama wanaotembea kivyake wakati wote isipokuwa wakati wa kupandana tu.

1. Nyegere ana gozi gumu zaidi kuliko haywani wte wa mwituni kiasi ambacho ni ngumu sana kumuua kwa mshale au hata panga, gozi la mnyama huyu linafanua sindano ya nyuki kudunda tu....anasaidiwa kucha zake, ndefu na ngumu awapo katika hatari ya kushambuliwa ngozi yake huwa ngumu na kukakamaa zaidi ("defensive mechanism).
2. Nyegere hula vyote iwe nyama iwe majani na hii imemfanya kustahili shuruba za mazingira yote iwe nyikani ama mwituni. Chakula chake kikubwa ni asali, yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula.

Nyegere hula nyoka wa aina yoyote, ana sumu kali ambayo akimng'ata nyoka wa aina yoyote haponi ingawa wapo nyoka wenye sumu ambao Nyegere akiwala anaweza kuzimia kwa msaa kadhaa kutokana na ukali wa sumu ambayo inakuua wewe kwa dakika tu.

3.Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa dunianikwani ana wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari, maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike.......Wivu wa Nyegere hufanya awachukie sana binadamu wanaume, mwanaume ukiwa porini ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano, huona wivu kuwa utamtamani jike, hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.
4. Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere, anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke, mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake (ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii
Ogopa sana kukutana na mnyama mwenye wivu Nyegere...

Yasemekana huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja, akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya.

Geofrey Chambua kutoka vyanzo mbalimbali 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hehehehe huyu mnyama kiboko

    ReplyDelete
  2. Safi sana.....ila namba tatu kiboko......hata jani hahahhahahahaha

    ReplyDelete
  3. usithubutu kukutwa na Nyegere

    ReplyDelete
  4. wale warina asali habari ndiyo hii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...