THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MKURUGENZI IDARA YA MAAFA APOKEA MIFUKO 640 YA SARUJI KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA MAAFA KAGERA.

Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia.Jen Mbazi Msuya (wa kwanza) akisalimiana na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal ltd Bw. Gagan Gupta wakati wa uhakiki wa misaada ya saruji iliyotolewa na kampuni hiyo kwaajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera tarehe 28 Oktoba, 2016.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen Mbazi Msuya (wa kwanza kushoto) akieleza jambo wakati alipotembelea ofisi za kampuni ya Kamal ili kupokea na kuangalia saruji zilizokabidhiwa na ofisi hiyo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal ltd Bw. Gagan Gupta (wa kwanza kulia) akizungumza jambo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu walipofika katika ofisi hizo kuangalia msaada wa safuji mifuko 640 unaosafirishwa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia.Jen Mbazi Msuya akiwa na Meneja Rasilimaliwatu wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal Bw. Ajay Jha wakati wa kuangalia saruji iliyotolewa na kampuni hiyo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera Oktoba 28, 2016.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal ltd wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen Mbazi Msuya mara baada ya kuangalia msaada wa saruji mifuko 640 uliotolewa na kampuni hiyo tayari kwa kusafirisha mkoani Kagera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)