NA K-VIS MEDIA, MOSHI
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio, ametembelele kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Oktoba 9, 2016, ili kuona eneo ambalo kitajengwa kiwanda kipya na cha kisasa.
Bw. Erio ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Steven Alfred, na Meneja Uhusiano, Bi.Lulu Mengele, pia alipata fursa ya kupokea taarifa ya uendeshaji wa kiwanda cha sasa na changamoto zinazokikabili. Bw. Erio alisema, ziara yake inalenga kujua mambo mawili ambayo ni kuona eneo patakapojengwa kiwanda kipya cha kutengeneza bidhaa za ngozi, lakini pia kupata uelewa wa nini kifanyike ili kuboresha kiwanda cha sasa ambacho kilijengwa mwaka 1977.

Maafisa wa kiwanda hicho, walimuonyesha maeneo mawili ambayo yanafaa kujengwa kiwanda hicho. “Kama mtakumbuka, wiki iliyopita mimi na Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), John Minja tulisaini makubaliano ya ushirikiano kati ya PPF na Jeshi la Magereza katika kukiboresha kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga, lakini pia kujenga kiwanda cha kisasa cha kuchakata ngozi na kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi.” Alianza kwa kusema.
Alisema, nia ya Mfuko ni kuona kazi ya ujenzi wa kiwanda kipya inakamilika ifikapo Desemba 2018 ili kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda. “Wakati tukisubiri ujenzi wa kiwanda kipya ukamilike, lazima pia tuboreshe hiki cha sasa kwa kuimarisha miundombinu iliyopo, na hivyo kuongeza uzalishaji na kupanua masoko ” alisema Bw. Erio.

Aliagiza wataalamu wa PPF kwa kushirikiana na wenzao wa Magereza (kiwanda cha Karanga), wakutane haraka ili kuainisha chamngamoto zinazokikabili kiwanda cha sasa, ili uboreshaji wa mitambo uweze kufanyika kwa haraka.” Alifafanua. 



Mkuu wa gereza la Karanga, mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro, ambako ndiko kilipo kiwanda cha kutengeneza viatu, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP), Hassan Bakari Mkwiche, (kushoto), akionyesha kitu, wakati Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (wakwanza kulia), alipotembelea kiwanda hicho ili kuona eneo lililotengwa kwa ujenzi wa kiwanda kipya cha kisasa cha viatu, Oktoba 9, 2016. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, (wapili kushoto), Mkuu wa magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP), Anderson Kamtera.
Bw. Erio, na maafisa wake, wakipatiwa maelezo na maafisa wa Jeshi la Magereza alipokagua moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho

Kamishna wa Magereza, (CP), Editha Malya, aliyemuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, (CGP), akizungumza wakati wa kikao cha kupeana taarifa na ujumbe wa PPF ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Erio Oktoba 9, 2016


Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. Erio, na Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Alfred, wakiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...