Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji, Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathon Mmuni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (Kulia) na Kushoto ni Manaja wa Maendelezo wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), James Oigo.

WADAU wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wanakaribishwa katika mkutano wa sita wa shirika hilo utakaofanyika Oktoba 20 na 21 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa (AICC) Arusha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji, Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathon Mmuni amesema kuwa maandalizi ya mkutano huo yanakaribia kumalizika kwahiyo  waajili na wadau wote wanaopenda kuhudhuria mkutano huo wanaombwa waendelee kujiandikisha katika Mtandaoni kupitia Tovuti ya www.nssf.or.tz. kabla ya Oktoba 18.

Amesema kuwa washiriki watatumiwa namba ya uandikishwaji kwenye Barua pepe zao(Email) namba hiyo itarahisisha utambuzi wa ushiriki wa mkutano huo,amesema kuwa  washiriki wa mkutano huo watajigharimia usafiri na malazi wawapo Arusha.
 Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji, Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathon Mmuni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mkutano wa wadau wa Mfuko huo utakaofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) Oktoba 20 na 21 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...