Na Luteni Selemani Semunyu,  JWTZ

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Brigedia Jenerali Davis Mwamunyange ambaye ni Mlezi wa Klabu ya Jeshi  ya  Lugalo Golf Club  ameimarisha safu ya uongozi wa klabu hiyo kwa kuwateua Naibu katibu Mkuu na Mkuu wa Miundombinu kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

Jenerali Mwamunyange amemteua Kanali Rajabu Mohamed Mwenyumbu kuwa Naibu Katibu wa klabu na Kapteni Kitego Kuwa Mkuu wa Miundombinu ya Klabu(Ground Member) kuchukua nafasi ya Kanali Jackson Nsigaye aliyehamia Bukoba kikazi.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti wa Klabu hiyo Generali Michael Luwongo alisema  Hatua hiyo inalenga kuboresha klabu hiyo ambayo inamikakati mikubwa ya kuboreshwa na kuwa kitovu cha Michezo cha kisasa che nye hadhi ya Kimataifa.

Wakati huo huo wachezji wa Timu ya Golf ya  Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo ya  Jijini Dar es Salaam wako katika maandalizi ya mwisho kujiwinda na Mashindano ya  Arusha open yanayotarajiwa kufanyika Hivi karibuni Jijini Arusha.

Akiongea na Waandishi wa Habari katika Klabu hiyo Kapteni Japhet Masai alisema mashindano  hayo ambayo ni muhimu katika kupandisha viwango vya wachezaji yanatarajiwa kufanyika  Jumamosi na Jumapili ya Oktoba 15 na 16 huku ikihusisha wachezaji wasio wa kulipwa (Amature).

Alisema Klabu ya Lugalo inatarajia kuingiza wachezaji  wa Daraja la A,B,C senior huku  wachezaji watoto ambao ni Junior watashindwa kushiriki kutokana na kuwa mashuleni katika kipindi hichi.

“ Mashindano haya ni Muhimu kwa Wachezaji wetu lakini pia itatupa fursa kwa wachezaji wetu wenye viwango kupata nafasi kuchezea timu ya Taifa iwapo wataonekana. Alisema Kapteni Masai.

Kapteni Masai alisema kumbukumbu ya Matokeo mazuri katika mashindano ya Tanzania open  kwa kuchukua ushindi wa Kwanza na wa Pili gross huku Daraja B ikichukua Ushindi wa Kwanza na katika mashindano ya Moshi Open kuchukua nafasi ya Kwanza Mshindi wa Jumla.

Kwa upande wake  Afisa Utawala wa Klabu hiyo Kapteni Amanzi Mandengule alisema Jumla ya wachezaji 10 wanatarajiwa kwenda kushiriki michuano hiyo wakiwemo wanawake watatu na wanaume Saba.

Aliongeza kuwa kikosi cha wachezaji hao Kitaongozwa na  Kapteni Amanzi Mangengule, Kapteni Japhet Masai, Kapteni Kibuna Shabani, Juma Likuli,Noel Mheni,Nicolous Chitanda ,Michael Obare, Amina Hamisi,Sara Denis  na Sophia Mathias.

Afisa huyo wa Utawala alisema maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni Baraka za Mwenyeki wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo ili kuhakikisha wanakwenda kuwakilisha vyema  Jeshi kwa kurejea na Ushindi.
 Mpiga Golf Sara Denis Amina wa Klabu ya Golf ya Lugalo Jijini Dar Es Salaam akiwa katika Mazoezi  kujiwinda na Mashindano ya Arusha Open yanayotarajiwa kufanyika Hivi karibuni Jijini Arusha Nyuma ni Amina Hamisi,Sophia Mathias wachezaji wenziei wa klabu hiyo


 Nahodha  wa Klabu ya Golf ya Lugalo Kapteni Japhet Masai (katikati) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Operation na Mafunzo wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu(OTO) Brigedia Jenerali Jairos Mwaseba alipotembelea viwanja vya golf vya Lugalo Jijini Da r es Salaam katika mashindano ya CDF Trophy 2016.
 Mnaadhimu Mkuu Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzani Luteni Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) Akisalimiana na Meneja wa Klabu ya Golf Lugalo Kanali Gerlard Omary, alipowasili katika Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam kusuhudia mashindano  ya Mkuu wa majeshi yaliyomalizika hivi karibuni Katikati ni Mwenyekiti wa klabu hiyo Brigedia Jenerali Michaele Luwongo
 Mnaadhimu Mkuu Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzani Luteni Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) Akisalimiana na Mwenyekiti wa klabu Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michaele Luwongo mara alipowasili katika klabu hiyo Jijini Dar es Salaam kushuhudia CDF Ttophy iliyomalizika hivi karibuni.
Baadhi ya Wachezaji Wanawake wa Klabu ya Golf ya Lugalo ya Jijini Dar es Salaam wakiwa katika Mazoezi kujiwinda na Mashindano ya Arusha Open yanayotarajiwa kufanyika Hivi karibuni Jijini Arusha ( Picha na Luteni Selemani Semunyu) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...