Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela leo amezindua kampeni ya kuwanywesha watoto dawa ya Kinga tiba kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya  kichocho kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani Iringa. Shule zote za msingi katika wilaya ya Iringa zitapata dawa na kuwanywesha watoto wote ilikujikinga na ugonjwa wa kichocho. 

Mh Kasesela alisema ” wazazi wawa ruhusu watoto wao kupata kinga tiba kwani wataondokana na ugonjwa hatarishi. wataalamu wametuambia hazina madhara yoyote ili mradi mtoto awe amekula”. Shule zote zitakazo toa dawa zitahakikisha watoto wana pata chakula kabla hawajapewa.
Zoezi hili litafanyika kwa wiki  mbili na kuhakikisha kila mtoto anapata Kinga tiba
a1
Pichani mbalimbali zikionyesha Mkuu wa wilaya akiendesha zoezi la kugawa dawa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Umsalaam iliyopo manispaa ya Iringa. Pia alipatafursa ya kuwafafnunulia baadhi ya wazazi waliokuwa na shaka na dawa hizo . 
 a3 a4

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...