HATIMAYE waimbaji wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab kwa hivi sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid watapambana vikali leo Oktoba 22 ndani ya ukumbi Dar Live Mbagala. Unaambiwa ni malkia wawili ndani ya jukwaa moja, ambapo Isha Mashauzi atathibitsha kuwa nyeye ni malkia wa masauti matamu huku Leyla akitaka kudhihirisha kwamba yeye ndiye malkia wa taarab. 
 
Bendi mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla. Waimbaji hao wawili kwa pamoja wameuthibitishia mtandao huu kuwa baada ya majigambo mengi kutoka kila pande, leo mzizi wa fitna utakatwa ndani ya Dar Live. 
 
Leyla Rashid amesema anamsikitikia sana Isha Mashauzi kwa kukubali kushiriki mpambano huo kwa vile kwasasa yeye (Leyla) ni maji marefu ambayo kamwe Isha hawezi kuyagoka. Naye Isha Mashauzi ametamba kuvuna ushindi mkubwa na kuongeza kuwa Leyla ameingia choo cha kiume kwa kukubali mtanange huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...