Shindano dogo la kumtafuta mrembo mwanamitindo TOP MODEL limefanyika mkoani Arusha Jumamosi iliyopita huku mrembo wa Sinza Sia Pius kutoka Kanda ya Kinondoni akiibuka mshindi katika shindano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha.

Jumla ya warembo 30 walipanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo ni la pili kushindaniwa kati ya Mataji 5 yanayo shindaniwa kabla ya shindano kubwa la Fainali za Miss Tanzania lililopangwa kufanyika jijini Mwanza tarehe 29 Oktoba 2016.

Washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wameingia kambini tangu tarehe 30 Septemba 2016 jijini D’salaam , na baadae kuanza ziara rasmi ya kutembelea mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha na kumaliza ziara yao jijini Mwanza.

Wakiwa Makao Makuu ya Chama na Serikali mkoani Dodoma warembo hao 30 walishiriki katika shindano dogo la kumtafuta mrembo anaevutia katika picha. (Miss Photogenic) ambapo mrembo wa Dodoma Anna Nitwa aliibuka mshindi katika shindano hilo akifuatiwa na Sia Pius kutoka Kanda ya Kinondoni.

Washindi hao 2 Miss Photogenic Anna Nitwa na Top Model Sia Pius tayari wamejipatia tiketi ya kuingia katika hatua ya pili ya nusu Fainali (Top 15) huku mataji mengine 3 bado yanagombaniwa na washiriki hao 30

Mashindano hayo madogo yaliyobaki ni

Mrembo mwenye kipaji – Miss Talent

Mrembo mwanamichezo – Top sports woman

Mrembo chaguo la watu – Miss Personality

Mataji hayo madogo yote yatashindaniwa jijini Mwanza wiki hii kabla ya Fainali za Taifa zilizopangwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2016. Katika ukumbi wa Rock City Mall uliopo jijini Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...