Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Serikali kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) imeendelea kutekeleza uunganishwaji wa mtandao wa Mawasiliano wa Serikali ambapo mpaka sasa Taasisi 72 zimeunganishwa na mtandao huo. Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano eGA Suzan Mshakangoto alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miundombinu ya Tehama inayohusisha Serikali, leo Jijini Dar es Salaam.
Suzan amesema kuwa Taasisi za Serikali zilizounganishwa na mtandao huo zitakuwa zinawasiliana kwa gharama ndogo kwa kutumia simu zitakazokuwa zikitumika kama ‘extension’ ambazo zitakuwa zinatumia internet kupitia Mkongo wa Taifa. “Mtumishi wa Taasisi moja katika taasisi zilizounganishwa na mtandao huo anaweza kupiga simu kwenda taasisi nyingine ya nje ikawa kama amepiga simu ya ‘extension’ ndani ya ofisi moja,” alifafanua Suzan.
Vile vile Taasisi za Serikali zitapunguza gharama za kuchajiwa huduma za internet kutoka kwa watoa huduma binafsi ambao gharama zao ziko juu ukilinganisha na huduma inayotolewa na wakala wa Serikali. Aidha Taasisi na Idara zote za Serikali zitakuwa ndani ya mtandao na mtoa huduma mmoja wa huduma za mtandao ambapo itasaidia kwenye utunzaji wa nyaraka za Serikali na kurahisha mawasiliano ndani ya taasisi hizo.

Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Bi. Suzan Mshakangoto akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu matumizi ya Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali leo Jijini Dar es Salaam. Taasisi 72 za Serikali tayari zimekwishaunganishwa na Mtandao huo kupitia Mkongo wa Taifa. 
: Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Bi. Suzan Mshakangoto akiongea na mtu kutoka Taasisi ya Uongozi wa Elimu (ADEM) ya Bagamoyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matumizi ya Simu zilizounganishwa na Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija, MAELEZO. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...