THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mtendaji wa Kata aswekwa Rumande kwa Matumizi mabaya ya Fedha za Umma


Nteghenjwa Hosseah – Longido

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Londifo, Juma Mhina ameamuru polisi wa Wilaya hiyo kumkamata na kumuweka ndani Mtendaji wa Kata ya Gilai Lumbwa, Paul Lucas baada ya kutuhumiwa kutumia Fedha za umma vibaya zilizochangwa na wananchi wa maeneo hayo kwa ajili ya kuinua Sekta ya Elimu.

Agizo hilo la Mhina lilifanikiwa baada ya mara kwa mara kushindwa kumkamata Paulo baada ya kumkwepa kila alipokuwa akitafutwa na hatimaye mtendaji huyo kujitokeza kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisgo Gambo uliofanyika kwenye Kijiji cha IIchang Sapukin kata ya Gilailumbwa.

Mmoja kati ya wananchi walioshirki Mkutano huo Bi. Anni Mollel alimshukuru Rc Gambo kufika Kijijini hapo na kujionea hali halisi ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ambayo wananchi walichanga Fedha zao zaidi ya Tsh Mil 96 ila hazikutumika kama ilivyokusudiwa badala yake viongozi wa Serikali na Wenyeviti wa Kijiji walitumia Fedha hizo kujinufaisha binafsi badala ya kuwasaidia watoto kukaa kwenye mazingira mazuri ili wapate Elimu.
   Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro wakionyesha  zana  walizotumia kutengeneza barabara  ya Km 24 kwa nguvu zao wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Mrisho Gambo  katika  Kijiji hicho.
  Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro wakishangilia Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ulipokuwa unawasili katika Kijiji hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(Mbele kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo(Mbele  Kulia) wakiwasili  kwenye Mkutano wa hadhara  katika Kijiji cha  Esokonoi.