Neema Mwangomo, MNH

Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa kifaa maalumu cha kusaidia kuimarisha utendaji wa misuli (training balance and coordination). Msaada huo umekabidhiwa na Profesa Henrik Hautop Lund kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Denmark Copenhagen.Profesa Henrik amesema Fiziotherapia Utengamao ni moja ya matibabu ya misuli iliyoathiriwa na magonjwa yaliyoathiri ubongo kutokana na kiharusi au mtindio wa ubongo kutokana na majeruhi wakati wa kuzaliwa.

Profesa Henrik amekuwa na ushirikiano wa kiutafiti wa utengamao na Dk Khadija Malima ambaye ni Mtafiti Kiongozi ( Afya) kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia. Utafiti huo unahusu vifaa (Tiles) vya teknolojia ambayo hutumika kutibu misuli, mwendo na kuchangamsha akili kwa watoto wenye mtindio wa ubongo wa kiasi.“Vifaa hivi humwezesha mgonjwa kufanya mazoezi na pia kufurahia kama mchezo, hivyo wateja wanufaika ni wale wenye kiharusi waliopata ajali na hawawezi kutembea, lakini wanahitaji kuimarisha misuli.

“Lengo ni kufanya utafiti utakaothibitisha faida ya teknolojia hii ili kusambaza huduma ya matibabu ya utengamao sehemu zote nchini hata kwenye jamii kwani teknolojia hii inatumia betri kuchaji na inakaa saa 20,” amesema Dk Malima.Pia teknolojia hiyo imetolewa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Inuka Rehabilstiona centre.
Kutoka kushoto ni Mtafiti Kiongozi wa Afya katika Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk Khadija Malima na Profesa Henrik Hautop Lund wa Chuo Kikuu cha Denmark Copenhagen wakikabidhi kifaa maalumu cha mazoezi ya fiziotherapia utengamao kwa Physiotherapist, Abdalah Raphael Makala na Kaimu Mkuu wa Idara ya Physiotherapy katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Alex Gomwa.
Mmoja wa watoto wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akifanya mazoezi ya fiziotherapia utengamao leo.

Mmoja wa watoto wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akifanya mazoezi ya fiziotherapia utengamao leo.
…………………………………………………………

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tanzania Bwana? Kifaa hicho unanunua hata kwenye maduka ya michezo tu kinatangazwa kama maajabu!!! Kweli tutafika? Mzungu katuvunga hapo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...