Na Beatrice Lyimo-MAELEZO,Dar es Salaam.

SERIKALI imesema muswada wa sheria ya huduma ya habari utatoa fursa kwa vyombo vya habari kuiomba radhi jamii radhi kwa jamii pindi wanapoandika habari zenye upotoshaji na hawatochukuliwa hatua za kisheria kutoka katika mamlaka zinazohusika.

Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake katika vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas alisema hakuna haja ya waandishi wa habari kuuhofia muswada huo kipengele na badala yake wausome na kuelewa na kisha watoe maoni yao ili kuuboresha zaidi.

“Sifa moja ya taaluma ya habari ni kufuata maadili hivyo muswada umetoa fursa kwa mwanahabari kukanusha na kueleza ulichokosea hivyo mwandishi hatashtakiwa endepo akiona amekosea na kusahihisha ikiwemo kuomba radhi” alifafanua Mkurugenzi Abbas.

Kwa mujibu wa Abbas alisema kutakuwa na bodi maalumu itakayosimamia masuala ya maadili kwa waandishi wa habari nchini na hivyo kutoa fursa kwa waandishi hao kuhojiwa na kutoa ufafanuzi wa jambo husika.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akifanya mahojiano ya kipindi maalum cha heloo Tanzania kinachorushwa hewani na kituo cha redio Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini humo. Kushoto ni mtangazaji wa kipindi hicho, Sheila Simba.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akibadlishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Redio Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam, Angel Akilimali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo ya ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (katikati) akizungumza na wahariri na waandishi wa gazeti la Uhuru wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo, Ramdhani Mkoma na kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara Habari( MAELEZO), Jonas Kamaleki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...